KISHAPU WALIA NA SHIDA YA MAJI. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

KISHAPU WALIA NA SHIDA YA MAJI.

Mchuuzi wa maji Kijiji cha Mhunze akichota maji kwaajili ya kuuza. Dumu moja huuza wastani wa sh 500.
 
Wanyama anuai wakinywa maji kwenye chanzo cha maji ambacho hutumiwa pia na wanakijiji

Mtoto akichota maji katika kisima cha muda Mto Tungu, kijijini Mhunze.

Mashimo haya ni visima vya muda ambavyo kwa sasa vimekauka katika eneo la Mto Tungu.


Wanafunzi nao baada ya shule hurudi mitaani na kusaidia familia zoezi la utafutaji maji.

NA THE HABARI
WANASEMA maji ni uhai, kinyume chake bila maji hakuna uhai wa  mwanadamu na hata wanyama. Kimsingi kauli hii inaonesha umuhimu wa maji  katika maisha ya kila siku ya binadamu na hata viumbe wengine. Shughuli nyingi zinazofanywa na mwanadamu kila siku zinategemea uwepo wa maji. Matumizi ya maji kwa shughuli za binadamu hayaepukiki. Na hata katika mwili wa binadau ni muhimu zaidi, kama huto yaitaji maji kwa  kunywa utayahitaji kwa kuoga na usafi wa shughuli nyingine.

Kwa mantiki hiyo hali yoyote ya upatikanaji ngumu ya upatikanaji wa  maji unaathiri maisha ya kila siku ya mwanadamu. Shida ya huduma ya maji eneo fulani huweza kuchangia ugumu wa maisha kiasi fulani. Shida ya  maji maeneo mengine huweza kupunguza shughuli za uzalishaji mali, hii ni kutokana na muda mwingi kupotezwa na jamii kwa ufuatiliaji wa maji hasa maeneo ya vijijini.

Hali kama hii ya shida ya huduma ya maji ndiyo inayowakumba wananchi  wa vijiji anuai vya Kata ya Kishapu, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Kata ya Kishapu ina vijiji nane yaani Mhunze, Lubaga, Isoso, Mwanuru,  Migunga, Mwamagembe, Mtaga, na Kishapu yenyewe.

Japokuwa vijiji vingi vina shida kubwa ya huduma za maji, lakini hali ya ugumu wa upatikanaji huduma hizo hutofautiana kutoka kijiji kimoja  hadi kingine. Kati ya vijiji vyote nane vijiji vinne ndio vyenye shida  ya maji zaidi. Vijiji hivyo ni pamoja na Lubaga, Isoso, Mwanuru na  Kishapu yenyewe.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages