Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi, akizungumza na wana habari, kuhusu kutunukiwa cheti 9001:2008 na shirika la viwango la kimataifa (ISO) baada ya kukidhi vigezo vya shirika la Det Norske Veritas (DNV)
linaloaminika kimataifa katika kutoa huduma za ukaguzi na uhakiki wa
utendaji wa viongozi na wafanyakazi katika makampuni, mkutano huo
ulifanyika jana katika ofisi za Kiwanda cha bia cha Serengeti
jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi wa uzalishaji na
usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor .
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti
Mark Taylor pamoja na Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul
Kitambi wakionesha cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la
Kimataifa(ISO) kwa wana habari jana katika ofisi za kiwanda cha bia cha
Serengeti jana jijini Dar es Salaam.
Meneja mawasiliano ya ndani wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Imani Lwinga
akizungumza jambo katika mkutano na wana habari jana jijini Dar es
Salaam.
Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi akiwa amebeba
cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) mara
baada ya kumaliza mkutano na wanahabari jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)