Mwenyekiti wa Baraza la michezo
Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi zawadi ya mshindi wa Pool
wanaume,Said Mohamed (kulia) wa Chuo
Kikuu Ruaha (RUCO) mara baada ya kuibuka bingwa katika fainali hizo.
Katikati ni meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo
Na
Mwandishi Wetu.
CHUO kikuu cha Biashara(CBE), jana
kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashidano ya mchezo wa pool Taifa kwa wanafunzi
wa vyuo vikuu yakijulikana kwa 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition
2013' baada ya kukifunga chuo kikuu cha Mzumbe Mbeya magoli 13-5 katika mchezo
wa fainali ya mashindano hayo.
Mashindano hayo ambayo mgeni
rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania(BMT), Dionis Malinzi,
yalifanyikia kwenye wa Viwanja vya Leaders Club mwishoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam.
Jumla ya vyuo vikuu vinane kutoka
katika mikoa minane ambavyo vilipatikana baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa vilishiriki
mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia yake ya Safari Lager.
Vyuo hivyo ni Ruaha Universititi
College(RUCO) kutoka Iringa,Mzumbe University(Mbeya Campus College) kutoka
Mbeya,Mzumbe University-Morogoro,St.John University-Dodoma,Moshi University
College of Co-operativeand Business Studies(MUCCOBS) kutoka Kilimanjaro,Institute
of Accountancy Arusha(IAA) kutoka Arusha,mabingwa wa mwaka jana St.Augustine
University of Tanzania(SAUT) kutoka Mwanza na wenyeji wa mashindano College of
Business Education(CBE) ya Dar es Salaam
Chuo cha CBE kwa kutwaa ubingwa huo kwa
mwaka 2013 kilijinyakulia Kombe na fedha taslim Sh.2,500,000 ambapo mshindi wa
pili Mzumbe Mbeya kilizawadiwa fedha taslimu Sh.1,500,00.
Chuo cha Mzumbe Morogoro kilichukua
nafasi ya tatu kwa kuwafunga mabingwa watetezi SAUT 13-8 na hivyo kujinyakulia
fedha taslim Sh.1,300,000 na mshindi wa nne akawa SAUT ambaye alizawadiwa fedha
taslim Sh.1,000,000.
Vyuo vinne vilivyotolewa kutoka katika
mikoa mine ambavyo RUCO-Iringa,St.John Dodoma,MUCCOBS Kilimanjaro na IAA Arusha
vilipewa kifuta jasho cha Sh.500,000 kila chuo.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja
(wanaume), Said Mohamed kutoka chuo cha RUCO Iringa aliibuka kuwa bingwa na
kuzawadiwa fedha taslimu Sh.300,000 baada ya kumfunga George Titto wa SUA Morogoro
ambaye ndiye mshindi wa pili alizawadiwa Sh.200,000.Mshindui wa tatu ni Patrick
Peter kutoka chuo cha IFM ambaye alizawadiwa Sh.150,000 na wanne ni Walter
Thomson wa TEKU Mbeya ambaye alizawadiwa Sh.100,000.
Udande wa wanawake, Lilian Meoli wa
chuo cha CBE Dar es Salaam alifanikiwa kutwaa ubingwa na kujinyakulia fedha
taslimu Sh.200,000 baada ya kumfunga Agnes Jacob wa chuo cha CBE Mwanza 2-0
ambapo Agnes alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa Sh.150,000.Mshindi wa tatu
ni Amina Mhina wa chuo cha Mzumbe Mbeya alizawadiwa Sh.100,000 na wan ne Lemi
Jaksoni kutoka St.Anthon Dodoma ambaye alizawadiwa Sh.50,000.
Kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi,
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania,Dionis Malinzi aliwapongeza
wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, bia ya Safari Lager kwa kuweza
kuuinua mchezo huo na kuufikisha hapa ulipofika.
Malinzi pia aliwapongeza viongozi wa Chama
cha Pool kuanzia mikoa hadi taifa kwa
ushirikiano wao ambao umeendelea kumvutia mdhamini kuendelea kuudhamini
mchezo huo bila ya kurudi nyuma..
"Ni vema mkaendeleza amani na
ushirikiano mlionao sasa ili mchezo wa pool uendelee kumvutia kila Mtanzania.
Nakwa upande wa serikali inautambua
kama ilivyo michezo mingine na Baraza la michezo itaendelea kuwaunga mkono
katika kuuendeleza zaidi ili siku moja uweze kuiletea heshima Tanzania katika
mashindano ya kimataifa,"alisema Malinzi.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)