Mheshimiwa
Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge
na NMB kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate.
Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki
saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka
kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote
zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.
Timu
ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati
yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya
Jamhuri hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB
imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata
na shoka ambao
umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)