BENKI YA NMB YA ZINDUA CHAP CHAP AKAUNTI KWA AJILI YA WATANZANIA WASIO NA AKAUNTI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

BENKI YA NMB YA ZINDUA CHAP CHAP AKAUNTI KWA AJILI YA WATANZANIA WASIO NA AKAUNTI



 Mh. Waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.




 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru Mh. Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap .


Sehemu ya maofisa wa NMB na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.
Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania. 

Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki  ya NMB ilizindua akaunti ya Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.

Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha  ndani ya dakika  kumi
·          Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:
Kuona Salio la Akaunti yako Popote pale ulipo
Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
  1.  Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
Kuchukua fedha hadi shillingi 1,000,000/= kutoka kwenye ATM  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages