Barclays Bank yaendesha droo ya pili ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Barclays Bank yaendesha droo ya pili ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake

image DSC_0599Tunu Kavishe, Communications Manager(centre) and Musa Kitoi Acting Consumer Retail Director in a picture with some of the winners of the Golden Briefcase Campaign during the 2nd Draw today
DSC_0616Khadija Kashoro and Anorld Shirima posed on a photo with their Golden Brifcase Gift after the 2nd Draw today, right is Tunu Kavishe Communications Manager

18 June, 2013 –  Barclays Tanzania leo imefanya droo yake ya  pili ya kampeni  ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake. Droo hii inawapa fursa wateja 13 kujishindia masanduku 13 ya dhahabu kwa muda wa miezi mitatu. 
 
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa benki, kitengo cha wateja  binafsi,  Bwana Musa kitoi alisema, “ Fursa ya ushindi iko wazi kwa kila mteja (Wateja waliopo na watarajiwa) mwenye akaunti na Barclays Bank Tanzania. Leo tumekamilisha droo yetu ya pili na tumewapata washindi 13. Vile vile tunatoa zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza iliyofanyika tarehe 22 Mei 2013, katika masanduku kumi na tatu ya dhahabu. Kila mteja atachagua sanduku na kulifungua ili kuweza kujua zawadi yake. Zawadi zilizopo ni i-Pad, Home theatre, Mashine za kufulia na vocha za zawadi. 
 
Bwana  Kitoi aliongeza na kusema kuwa “ukiweka pesa zako benki na ukawa na salio lililokusudiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia kwenye droo hii na utapata nafasi ya kujinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya tshs millioni kumi (10,000,000 TZS)” mwisho wa kampeni. Kampeni hii ilizinduliwa rasmi tarehe11 Aprili 2013 na itaendelea hadi tarehe 30th June 2013. 
 
Shindano hili liko wazi kwa  wateja  binafsi, wapya na wa zamani, ambao wanaweka fedha zao  na benki yetu hapa Tanzania. Wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hii ni wale tu wenye account ya hundi (Current Account)  au amana (Savings), na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye account kwa shillingi laki tano za kitanzania (500,000 tzs)au zaidi, na salio hili libakie kwenye account hadi mwisho wa mwezi bila kupungua, Kila ongezeko la shillingi Laki tano linampatia mteja ingizo la ziada katika katika droo ya mwezi husika.. 
 
Zawadi kubwa ya shilling million kumi za Kitanzania (shs. 10,000,000) itatolewa mwisho wa kampeni. Zawadi zote zitawekwa kwenye Barclays Golden Briefcase ambapo kila mshindi atatakiwa kuchagua mojawapo kisha kuifungua ili kujua alichojishindia.  Zawadi zinazoshindaniwa kila mwezi ni  iPads 2, vocha 8 za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shillingi laki 2 kila mmoja (TZS200, 000), mashine za kuoshea nguo 2, na home theatre 1.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages