Zantel yazindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wa Zanzibar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Zantel yazindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wa Zanzibar

Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa akionyesha baadhi ya zawadi zitazogombaniwa wakati wa promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’. Kulia kwake ni Awaichi Mawalla, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla.

Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, leo imezindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wake wake wa Zanzibar ikiwa ni katika juhudi zake za kuwazawadia wateja wanaotumia mtandao huo.

Promosheni hiyo kubwa ambayo mshindi wake atajinyakulia gari, itawazawadia wateja wengine zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni  moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.

Ili kushiriki katika promosheni hiyo, wateja wapya na wale wa zamani wa Zantel wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi ili kuingia kwenye droo hiyo.

Akizungumzia promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, alisema promosheni hiyo inathibitisha nia ya kampuni hiyo katika kuboresha maisha ya wateja wake huku wakiendelea kuwasiliana na ndugu na marafiki zao.

“Tuna furaha kubwa leo kuzindua promosheni hii kwa wateja wetu, ambayo hakika itawapa thamani ya pesa zao kwa kujishindia zawadi mbalimbali’’ alisema Mussa. Promosheni hii itaendeshwa kwa kipindi cha miezi miwili,
kuanzia leo tarehe 6 mwezi wa tano hadi tarehe 6 mwezi wa saba.

Kwa kipindi chote cha promosheni Zantel itatoa jumla ya modemu 60 za 3G, komputa ndogo 12 (Huawei Media pads), pikipiki 6, muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja pamaoja na gari moja.

“Promosheni hii itaipa kampuni yetu fursa ya kuwasiliana na wateja wetu, huku pia tukiwashukuru kwa kutumia huduma zetu’’ alisisitiza Mussa.

Wakati huo huo kampuni ya Zantel pia imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake wa nchi nzima, iitwayo ‘Bonus Balaa’ ambayo itawapa mara mbili ya muda wa maongezi wakiweka vocha ya kuanzia shilingi elfu moja au zaidi. Muda huo wa maongezi utawawezesha wateja wa Zantel kupiga mitandao yote.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages