Mei
15, 2013 Dar es Salaam, Jumatano iliyopita kupitia televisheni za ITV na Clouds
TV timu ya Ghana iliyoshinda katika kipindi cha Tisa cha GUINNESS® FOOTBALL
CHALLENGE walifurahia kupata nafasi katika nusu fainali kwa kucheza azonto
ambayo iliwafanya watangazaji Larry na Mimi kujiunga nao. Kofi Okarku na Isaac
Aryee ingawa hawakufanya vizuri katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa
Guinness walifanikiwa kupata dola za kimarekani 1,500 na waliufanya uwanja
wote kunyanyuka na kucheza.
Timu
iliyoshinda ilifanya vizuri katika hatua za mwanzo na kujipatia alama 16 pamoja
na kuonesha uwezo mzuri ufahamu wa soka. Waliwashinda Wakenya katika hatua ya
penati, hata hivyo timu ya Kenya imefuzu nusu fainali kama washindi wa pili.
Emanuel,
Kenneth, Chris na Isaac wataendelea kuziwakilisha nchi zao katika hatua ya nusu
fainali, wakiwa na ndoto za kufanya vizuri na kuwa washindi wa Pan-African Guinness Football
Challenge.
Meneja
wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi alisema, “Nusu fainali ya kwanza
inatarajia kufanyika wiki ijayo tukisubiri kuona ni nani atakayefanikiwa
kutinga fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Timu kutoka
Dar-es-Salaam,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad watapeperusha bendera ya
taifa letu na kuwakilisha Afrika mashariki hivyo tunawatakia kila la heri. Tunazisifu timu zote
na sasa timu bora zitakutana kuwania kufuzu kuingia fainali”
Timu
zitakazoendelea na michuano ni pamoja na;
KWA WATANZANIA
·
NDANI
YA JEZI ZA KIJANI-Kutoka Dar-es-Salaam, Daniel
Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao awali
walijishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya kitaifa na
waliishia katika hatua ya penati kwenye robo fainali wataweza kufikia hatua ya
pesa ukutani katika nusu fainali?
KWA WAKENYA
·
NYEUSI-Kenneth
Kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi.Ken ni kocha na Wills ni dereva.Timu
hii ilijishinda katika robo fainali ya pili na kuongeza dola 1,500 kwenye dola 3,000 walizokuwa nazo
awali.
· JEZI
NYEKUNDU-ni timu ya pili kutoka Kenya,Francis Ngigi
kutoka Nairobi na Kepha Kimani kutoka Thika.Timu hii ilipata dola 3,000 katika
hatua za kitaifa na walifika hatua ya penati katika robo fainali.
KWA WAGHANA
·
JEZI
ZA BLU- Timu ya Ghana iliyopata fedha nyingi zaidi
katika hatua ya kitaifa, Jonathan Naab kutoka Tindogo na Desmond Odaano kutoka
Larteh wamefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kupata jumla ya dola
8,500. Je, watafanikiwa kuingia fainali?
Nusu
fainali ya kwanzaitarushwa na televisheni za ITV na Clouds TV usikose kuangalia
mchezo huu na kushangilia timu yetu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football
challenge nchini wanaweza kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS®
VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa
kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa
kupitia simu ya mkononi.
Usikose kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya
kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia
na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya
bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa
wale wenye umri chini ya miaka 18.
Notes to Editors:
The GUINNESS and FOOTBALL
CHALLENGE, and GUINNESS VIP words and associated logos are trade marks
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)