TAARIFA ZISIZO RASMI ZINASEMA KUWA HAYATI NGWEA AMEFARIKI KWASABABU YA KUZIDISHA MADAWA YA KULEVYA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAARIFA ZISIZO RASMI ZINASEMA KUWA HAYATI NGWEA AMEFARIKI KWASABABU YA KUZIDISHA MADAWA YA KULEVYA.

429782_582455318465187_1421897743_n
Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.
DSC04280

 Akiongea na Clouds FM muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.
 
Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa kuwa Mangwea alikuwa pamoja na mtu aitwaye M TO THE P ambaye naye yupo mahututi kwa sasa.

“Sijui hata huko alitumia nini,” amesema.

Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.

Hata hivyo amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.

Awali Bongo5 ilizungumza na Bushoke anayeishi jijini Pretoria ambaye amesema alikuwa akutane naye leo jijini Johannesburg lakini alishangaa kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washkaji ambao ni wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki.

“Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke. Bushoke amesema kesho amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe. 

Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages