RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIWANDA VYA BIDCO OIL NA AZAM BUGURUNI DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIWANDA VYA BIDCO OIL NA AZAM BUGURUNI DAR

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mafuta yaliyowekwa virutubisho vya lishe bora wakati alipokitembelea kiwanda cha BIDC Oil and Soap kilichopo eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wadau wa lishe bora kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa  wakizindua mpango wa kuweka virutubisho vya lishe bora katika bidhaa za unga na mafuta nchini uliofanyika katika kiwanda cha BIDCO Oil and Soap kilichopo katika eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya kikwete akiangalia ukaguzi wa uwepo wa virutubisho vya lishe bora katika bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha kuzalisha unga AZAM ukifanyika katika maabara ya kiwanda  hicho Buruguruni jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha BIDCO Oil and Soap muda mfupi baada ya kuzindua mpango wa kuweka virutubisho bora vya lishe katika bidhaa za unga na mafuta uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Akihakiki jambo katika moja ya Kompyuta ya ofisi ya Kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages