“Natambua mimi ni mwanamuziki, sawa nina mashabiki wengi lakini
haina maana kwamba sina haki ya kuchagua chama ninachoona mimi
kinanifaa, lakini siwezi kusita kufanya kazi sehemu yoyote au wakati
wowote chama kikinitaka nifanye kwa wakati husika,” alisema Profesa J.
Profesa Jay amesema hakujiunga na CHADEMA ili mwaka 2015 awanie ubunge kama wengi wanavyodhani.
Rapper huyo wa ‘Machozi, Jacho na Damu’ ambaye jina lake halisi ni
Joseph Haule, ameliambia gazeti la Mwananchi la leo kuwa amejiunga na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili kukisaidia chama katika
changamoto za kuikomboa nchi.
“Kujiunga na siasa si dhambi na haina maana kwamba nina mpango
wa kugombea jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sihitaji kugombea
hata udiwani ila ni kwa dhumuni la kutaka kuongeza nguvu katika chama
ili kuyafikia malengo,” ameliambia gazeti hilo.
Ameliambia kuwa yeye ni mfuasi wa Chadema tangu mwaka 2005 na
amekuwa karibu na chama kwa nyakati nyingi lakini kwa sasa ameamua
kuingia rasmi katika chama kama chachu katika kuongeza harakati kwa
vijana.
“Nimeingia ili nisaidie hiki chama kuikomboa Tanzania kwani kwa
muda mrefu niliokaa katika chama hiki nimegundua kuwa wamedhamiria
kumkomboa msanii, kijana wa kawaida na wakubwa kwa wadogo hivyo nadhani
nipo sahihi katika uamuzi wangu.”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)