Dar
es Salaam: Mei 22, 2013 Juma tano usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV
tumeona nusu fainali ya kwanza ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLEGE™ ambapo timu ya
Ghana walionesha kuwa wao ni timu bora baada ya kushinda na kuwa timu
iliyoshinda kiasi kikubwa zaidi cha pesa.
Jonathan
Nabb na Desmond Odaano walionesha kuwa wana uwezo na ni majasiri walipowashinda
wapinzani wao na mwisho kushinda kitita cha dola za kimarekani 12,000 baada ya
kulenga kitundu namba nne katika hatua ya pesa ukutani.
Watakaorudi
nyumbani ni Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Dar-es-Salaam wakiwa na
na dola 5,500 walizojipatia katika hatua za kitaifa. Sasa kazi itakuwa kwa timu
mbili za Kenya katika nusu fainalli ijayo watakapokuwa wakiiwakilisha Afrika
mashariki.
Washindi
Jonathan na Desmond, walizawadiwa pia dola za kimarekani 4,000 baada ya
kuonesha mchezo mzuri sana katika mizunguko miwili ya mwanzo ya mchezo ambapo
hawakukosa hata swali moja. Sasa wamefanikiwa kuingia katika fainali ya
Pan-african na kujihakikishia na hata
kuwa washindi wa mashindano hayo.
Kutoka
Nairobi Kenya, Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao wameshika nafasi ya pili
wataungana pia na washindi wa kwanza Jonathan na Desmond katika hatua ya
fainali. Japokuwa hawakufanikiwa kufikia hatua ya pesa ukutani lakini wamefuzu kuingia
fainali. Wenzao kutoka Kenya Kenneth Kumau na Wills Ogutu hawakufanikiwa kufuzu
hivyo Francis na Kepha ndio watakaoiwakilisha Afrika mashariki.
Meneja
wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi alisema,”Sote Tanzania tunawapongeza
Daniel na Mwalimu-japokuwa hawakufanikiwa kufuzu fainali lakini wamejishindia kiasi kikubwa cha pesa. Kila
timu ilijitahidi kufikia nusu fainali na hongera kwa Desmond na Jonathan kutoka
Ghana kwa ushindi wao. Sasa tunasubiri nusu fainali ijayo kila la heri kwa wote
pamoja na timu za Kenya zitakazowakilisha Afrika mashariki”
Watakaoingia
uwanjani katiaka nusu fainali ya pili kuwania nafasi mbili za kucheza fainali:
AFRIKA MASHARIKI:
·
JEZI
NYEUSI – Ephatus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) kutoka
Nairobi watatarajia kushinda zaidi ya dola 3,000 walizopata katika hatua za
kitaifa na robo fainali. Ephatus atajibu maswali wakati Samuel anayechezea
Nakuru Allstars atakuwa akionesha uwezo wa kusakata kabumbu.
·
JEZI
NYEKUNDU – Kenneth Mukuri (26) na Chris Mwamgi (19)
kutoka Nairobi watakuwa wakitarajia kushinda zaidi ya dola 1,500 walizopata
katika hatua za kitaifa. Kenneth atakuwa kichwa cha timu wakati Chris atakuwa akionesha
uwezo wake wa kisoka
CAMEROUN:
·
JEZI
ZA KIJANI – Emerald Tchouta (24) na Abdul Sam (25)
ambao wana jumla ya dola 6,500 baada ya kulenga lengo namba nne katika robbo
fainali. Sasa Emerald na Abdul watacheza kuwania nafasi ya kufuzu fainali.
GHANA:
·
JEZI
ZA BLU – Emanuel Kofi Okarku (27) na Isaac Aryee (25)
kutoka Accra Ghana wataiwakilisha nchi yao kutoka Afrika magharibi ili kufuzu
fainali. Tayari wana dola za kimarekani 3,000 hivyo Isaac atahitajika kuonesha
kipaji chake cha kucheza soka wakati
Emanuel atajibu maswali.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guinness football challenge wanaweza kupima maarifa yao
katika soka kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure
kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia
simu ya mkononi.
Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Nusu fainali ya pili ya mashindano haya
imeandaliwa na kutengenezwa na Kampuni
ya kimataifa ya Endemol, na kurushwa na Televisheni ya ITV siku ya Jumatano saa
3:15 usiku, huku ukiburudika na bia yako ya Guinness.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa
wale wenye umri chini ya miaka 18.
Notes to Editors:
The GUINNESS and FOOTBALL
CHALLENGE, and GUINNESS VIP words and associated logos are trade marks
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)