MFANYABISHARA AJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA 9 KARIAKOO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MFANYABISHARA AJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA 9 KARIAKOO

Wananchi wakiangalia mwili wa aliyekuwa Mfanyabiashara wa katika moja ya maduka ya Kariakoo aliyetambulika kwa jina moja la Shirima, aliyejirusha kutoka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord ni leo mchana huu maeneo ya Kariakoo.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea, wameeleza kuwa walipatwa na mshuko mkubwa baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichoangua na kuhisi labda ni 'yale yale' ya maghorofa kuporomoka yenyewe baada ya kuguswa na Kunguru, kumbe ni mtu huyo aliyeanguja juu gari hilo.

Na baada ya watu hao kusogea eneo hilo walikuta ni mwili wa mtu aliyeanguka kutoa ghorofani ambaye baadhi yao waliweza kumtambua kwa jina moja kuwa ni Shirima.  Baada ya tukio hilo wasamaria wema wamemkimbiza mtu huyo hospitali kutokana na kwamba alikuwa bado akipumua

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia juu ya Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imeegeshwa nje ya hoteli hiyo. Haikuweza kufahamika chanzo cha jamaa huyo kujirusha kutoka ghorofani. Picha kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages