MEDIA DAY BONANZA LAFANA SANA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS HUKU TANESCO WAKIIBUKA WASHINDI WA MPIRA WA MIGUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MEDIA DAY BONANZA LAFANA SANA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS HUKU TANESCO WAKIIBUKA WASHINDI WA MPIRA WA MIGUU


 Muwakilishi kutoka benki ya NMB akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya TANESCO,mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika  bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group na kufanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Bonaza hilo lilijumuisha makampuni 14 na yote yalichuana vikali kuhakikisha kila mmoja anajitahidi kushinda ili kulinda heshima.Lengo la la bonanza hilo ilikuwa ni kuwaweka pamoja wafanyakazi wa kampuni mbalimbali ili waweze kufahamiana na pia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao.
Pichani kulia ni Meneja wa bia ya Castle Lager (TBL) kabula Nshimo akimkabidhi nahodha wa timu ya Fast Jet kikombe kwa kuibuka washindi wa pili katika bonanza la soka la Mei Mosi lililojulikana kwa jina la Sports Bar & Sports Xtra Day,lililoratibiwa na Clouds Media Group.
 Baadhi ya wachezaji  na washabiki wa timu ya Fast Jet wakishgalia kombe lao mara baada ya kunyakua nafasi ya washindi wa pili.
Mchezaji wa timu ya Clouds Media Group,Ben Kinyaia akiwatoka wachezaji wa timu ya TBL
 Mchezaji wa Fastjet aka Nafuu aka Kasuku akitoa pasi mbele ya wachezaji wa Infinity
 Mchezaji wa timu ya TANESCO akimchomoka mchezaji wa timu ya Fast jet,wakati wa fainali yao iliyowakutanisha pamoja,ambapo timu ya TANESCO waliibuka kinara kwa kuifunga timu hiyo ya Fast Jet goli 1-0,na hatimaye kunyakua kombe la ushindi katika bonanza hilo lililofana kwa kiasi kikubwa.
 Mchezaji wa Timu ya Infinity Communication akimkaba mchezaji wa timu ya Fastjet katika mashindano yaliyofanyika jana katika viwanja vya leaders
 Kiungo mchezaji wa timu ya Fastjet akiokoa mpira mbele ya mchezaji wa Infinity Communication
 Mlinda Mlango wa Infinity Communication akishuhudia mpiraa ukiingia nyavu kwake na kufanya timu ya Fastjet kuongoza kwa Magoli 2 kwa bila
 Wadau kutoka Infinity Communication Kutoka Kushoto Mgisha Lukaza akiwa na wafanyakazi wenzake katika viwanja vya leaders kushuhudia timu yao ya Infinity Communication katika bonanza la May Day lililofanyika katika viwanja vya leaders hapo jana
 Wadau wa Infinity wakilonga baada ya timu yao kufungwa magoli 2 kwa bila na timu ya Fastjet aka Nafuu aka Kasuku
Baada ya mpira wa miguu kuisha na kuwapata washindi,pia kulikuwepo na burudani iliyotolewa na bendi ya muziki wa dansi ya Skylight pamoja na wasanii mbalimbali kutoka THT.
Baadhi ya wakazi wa jiji la dar wakisubiri kushuhudia burudani kutoka kwa Bendi ya Skylight Band.Picha na Josephat Lukaza/Michuzi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages