MAJAMBAZI YAPORA ASUBUHI KWEUPE SAYANSI MATAA KIJITONYAMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAJAMBAZI YAPORA ASUBUHI KWEUPE SAYANSI MATAA KIJITONYAMA

 Pichani ndio matundu ya risasi zilivyorindima kwenye kioo cha dereva (risasi tatu) na kushoto risasi moja kama kionekanavyo kioo cha juu,mara majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana  kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi
mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano
kasoro. Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio
wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda  piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili  wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine  gun na wengine walikuwa na bastola.

Mmoja wao alifyatua risasi hewani  kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya  utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi  kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu  ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa  lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva  aliempeleka majeruhi hospitali),mara baada ya majambazi hayo kutimka  wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu  ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
 Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages