Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye
Mnara wa Mashujaa viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya
kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali
pamoja viongozi wa dini.
Mwakilishi
wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan
akiwasili kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye
maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa
Mataifa.
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi,
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw.
Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi akielekea
kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya
kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza
maisha wakiwa kazini.
Mh.
Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu
ya Mashujaa uliopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho
ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa mataifa walipoteza
maisha wakiwa kazini.
Mgeni rasmi Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara huo.
Mwakilishi
wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan
akielekea kuweka shada la maua kwenye maadhimisho ya kuwakumbuka Askari
wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo kwenye mnara wa
kumbukumbu ya Mashujaa uliopo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiweka shada la maua kwenye mnara huo.
Kanali
Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiweka shada la
maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya Meja Jenerali
Salum Mustafa Kijuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka Askari
wa kulinda Amani wa Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja leo.
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.
Mmoja
wa askari wa JWTZ akipendisha bendera ya Umoja wa Mataifa kama ishara
ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja huo wanaolinda Amani katika nchi
mbalimbali za Afrika.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa
mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi
wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan
akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini
Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa
Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
leo.
Zainab Abdallah moja ya Vilabu vya Umoja wa Mataifa akighani shairi wakati wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu
wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania
Bw.George Otoo (wa pili kulia) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia) wakiwa na baadhi ya maafisa
mbalimbali wa jeshi la Tanzania wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa
yakijiri kwenye maadhimisho hayo.
Kushoto
ni Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
na baadhi ya mabalozi na maafisa mbalimbali wa jeshi nchini.
Baadhi
ya Askari Wanawake wa Vikosi vya Kulinda Usalama wa Tanzania wakiimba
wimbo maalum wa kuhamasisha Amani katika maadhimisho hayo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akipeana
mikono na Askari Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani kutoka Tanzania
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi
wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan
akisalimiana na Askari wa Kulinda wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria
maadhisho hayo leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani kutoka Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akibadilishana
mawazo na mmoja wa askari wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda
Amani wakati wa maadhimisho hayo.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Na Mwandishi wetu.
Tanzania
imesema shughuli ya operesheni za kulinda amani katika mataifa yenye
mvutano wa kivita barani Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo upelekwaji wa wanajeshi na udhibiti wa rasilimali na utoaji wa
maamuzi.
Akizungumza
katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Walinda Amani wa
Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar e s Salaam, Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.
Emmanuel
Nchimbi amesema tunapoadhimisha siku hii pia tunawakumbuka raia, askari
na wapiganaji zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha tangu mwaka 1948 wakiwa
katika zoezi la kulinda amani.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania Bw. Richard
Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw.
Alberic Kacou amepongeza vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania na
Polisi wa Usalama wa Raia kwa kuandaa tukio hilo la kumbukumbu ya
walinda amani wa Umoja wa mataifa wake kwa waume waliopoteza maisha yao.
Amesema
katika siku hii ya kimataifa, tuitumie kuwakumbuka walinda amani zaidi
ya 3,100 waliopoteza maisha na kuwaunga mkono askari zaidi ya 111,000
waliopo na wanaoendelea kulinda amani katika nchi mbalimbali zilizo na
migogoro.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)