Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania, Phocus Lasway (kulia) akikabidhi vazi la suti mpya maalum kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakati wa hafla maalumu ya kuonesha vazi hilo la suti mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo,iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar. Wa pili kulia Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wakipita jukwaani huku wakiwa wamevalia suti hizo wakati wa hafla maalum ya kuonyesha mavazi yao hayo iliyofanyika jana jioni Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.
Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya
Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja.
Wadau wa soka nchini wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi suti mpya kwa Taifa Stars.
Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni mdhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) jana ilikabidhi suti mpya 30 za kisasa kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.
Suti hizo zilikabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa TFF Angetle Osiah na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa TBL, Phocus Lasway katika shughuli maalumu iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mpira. Shughuli hii pia ilitumiwa na Kilimanjaro Premium Lager kuiaga timu rasmi inapoondoka kwenda Ethiopia ili kujiandaa na mechi dhidi ya Morocco.
Wageni waalikwa walipata burudani ya aina yake pale ambapo wachezaji wenyewe pamoja na benchi zima la ufundi walipita mbele ya jukwaa kwa kujiamini ili kuonyesha suti mpya huku wakishangiliwa na pia watu waliokuwepo majumbani na sehemu nyingine walitoa maoni yao kwa njia ya twitter na facebook na maoni yao kuonyeshwa kupitia ‘scren’ kubwa zilizokuwepo ukumbini hapo.
Akizungumza katika tukio hilo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema wao kama wadhamini walipoanza kuidhamini Taifa Stars yapata mwaka mmoja sasa kwa kuwekeza zaidi ya bilioni 13 kwa miaka mitano, mojawapo ya jambo walilonuia kufanya ni kupandisha hadhi ya timu yetu na pia kuhakikisha ina mazingira mazuri ya kuleta ushindi.
Alisema suti hizo mpya zitawapa wachezaji wa Taifa Stars sura mpya kabisa kila wanaposafiri ndani na nje ya nchi kwani watafanana na wachezaji wengine wa kimataifa.
Alisema bali na suti hizo, wamefanya mambo mengine kama kukabidhi basi la kisasa kabisa la michezo ambalo limeiwezesha Taifa Stars kusafiri kwa raha kwani basi hilo lina uwezo wa kufanya safari hata za nchi jirani.
Aliwasihi wachezaji wajitume wanapoenda kuikabili Morocco katika mechi ya marudiano Mjini Marrakesh huku akisema Stars ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi hasa baada ya kuifunga Morocco 3-1 nyumbani.
“Ni matumaini yetu kuwa mutatupa raha zaidi kwa kuwafunga nyumbani kwao ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu,” alisema Bw Kavishe na kuwasihi wajiandae vizuri pia na mechi ya Ivory Coast itakayopigwa Dar es Salaam Juni 16.
Kwa upande wake, Rais wa TFF Leodgar alitoa shukrani kwa Kilimanjaro Premium Lager kwa kuwa mstari wa mbele kutekeleza mambo walioahidi kama wadhamini ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ari ya timu ya Taifa kufanya vizuri.
“Wametekeleza mambo waliyoahidi na kwa kweli hata wachezaji wanajiskia vizuri kuwa katika timu ta Taifa kwani wana uhakika wa kulipwa vizuri na kukaa sehemu nzuri wanapoingia kambini,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)