FM ACADEMIA KUSINDIKIZA UZINDUZI WA ALBAM RISASI KIDOLE YA MASHUJAA BAND JUMAMOSI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

FM ACADEMIA KUSINDIKIZA UZINDUZI WA ALBAM RISASI KIDOLE YA MASHUJAA BAND JUMAMOSI

Chaz Baba (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wakitangaza uzinduzi wa albam yao, utakaofanyika siku ya Jumamosi. Kushoto ni Mwimbaji wa Fm Academi, bendi itakayosindikiza uzinduzi huo, Nyoshi  El-Saadat (kulia) ni Rapa wa Mashujaa Band, Ferguson.

Na Mwandishi Wetu, Dar
BENDI ya muziki wa Dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma, inatarajia kusindikiza uzinduzi wa Albamu ya mpya ya Bendi ya Mashujaa itakayokwenda kwa jila la Risasi Kidole.
 
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii katika ukumbi wa Bissines Park Kijitonyama Jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wanamuziki wanaokubalika kwa sasa katika tasnia hiyo Chaz Baba (Mashujaa) na Nyosh El Sadat wa FM.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Chaz Baba ambaye ni Rais wa Mashujaa alisema, wamejipanga vya kutosha katika uzinduzi huo na ndio sabau kubwa ya kuwaomba FM kuwasindikiza ikiwa ni lengo la kuwapa burudani mashabiki wao.
 
“Tumejipanga sana, kutoa burudani nzuri nay a uhakika kwa wadau na mashabiki wetu watakaouzulia siku hiyo, kwani uzinduzi huo sio wa kitoto njooni mjionee wenyewe,”alisema Chaz.
 
Aidha Chaz aliongeza kuwa, albam hiyo inatarajiwa kuwa na nyimbo tisa huku huku akijitamba Raper wake kama Fergason kufanya makamuzi ya ajabu siku hiyo.
 
Naye Nyoshi alisema, kutokana na utu walionao na upendo ndiyo sababu iliyowafnaya kukubali ombi la Mashujaa nkuwasindikiza katika uzinduzi huo, na kudai kuwa siku za usoni hata wao wanatarajia kuwa na uzinduzi wa albam mpya huenda wakawaalika hata wao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages