Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barclays, Tunu Kavishe,
akizungumza na waandishi wa habari (hawao pichani), wakati wa uzinduzi
wa Matembezi ya Hisani ya Step Ahead Walk 2013 yatakayosindikizwa na
Barnaba na Kidumu.
*********************************
'Step
Ahead Walk’ ni mkakati endelevu wa Benki ya Barclays, ambao kusudi lake
ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii. Matembezi
hayo ya kila mwaka, yalizinduliwa mwaka 2008 hapa nchini na kusaidia
kuelimisha jamii kuhusu uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi
na afya ya watoto
KIBAO
cha ‘Wanawake,’ kilichoimbwa na nyota Bongo Flava Barnabas Elias,
akishirikiana na Mrundi Jean Pierre Nimbona ‘Kidumu,’ kimezinduliwa
rasmi leo na kutangazwa kupamba Matembezi ya Hisani ya ‘Step Ahead Walk
2013,’ yanayoratibiwa na Benki ya Barclays Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Mahusiano wa Barclays, Tunu Kavishe, alisema maudhui ya
wimbo huo ni kuhamasisha wadau kujitokeza kwa wingi kushiriki ‘Step
Ahead Walk’ ambayo lengo lake ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama
na watoto wachanga.
Aliongeza
kuwa, tukio hilo litafanyika Juni 8, 2013, katika hoteli ya Golden
Tulip, likihusisha matembezi ya hisani ya kilomita tano, ambapo kila mtu
katika jamii anakaribishwa kushiriki kwa kununua tiketi kwa silingi za
Kitanzania 5,000 ambazo zinapatika katika matawi ya Benki ya Barclays
kuanzia Aprili 29.
“Mwaka
2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kukusanya
shilingi mil. 150 kutokana na mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka
kwa wafadhili, lakini mwaka huu lengo ni kuchangisha mara mbili ya kiasi
hicho kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu na washiriki wengine
katika jamii,” alisema Kavishe.
Alibainisha
kuwa, kiasi kitakachochangishwa mwaka huu kitakwenda kusaidia katika
masuala ya uzazi na afya ya watoto, ikiwamo Mafunzo kwa wakunga wa
uzazi, matibabu ya Fistula na upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu
unaosababishwa na uzazi.
‘Step
Ahead Walk’ ni mkakati endelevu wa Benki ya Barclays, ambao kusudi lake
ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii. Matembezi
hayo ya kila mwaka, yalizinduliwa mwaka 2008 hapa nchini na kusaidia
kuelimisha jamii kuhusu uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi
na afya ya watoto.
Kavishe
alisisitiza kuwa, ‘Step Ahead Walk 2013’ itafanikiwa, kama tu
itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya Kitanzania, kwa hiyo
akawataka wadau kujiunga katika matembezi hayo ili kuweza kuleta
mabadiliko katika masuala ya afya ya Uzazi na Mtoto kwa ujumla hapa
Tanzania. Kwa Hisani ya Habari Mseto Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)