Mkuu
wa kitengo cha bidhaa Bwana.Samwel Mkuyu wa Barclays akionyesha mfuko
wenye kura za wateja wa benki hiyo wakati wa kuchezesha bahati nasibu
ya benki hiyo ya Maisha
Bomba na Barclays Golden Briefcase jana , katikati ni Tunu Kavishe Mkuu
wa kitengo cha mawasiliano na kushoto ni Hamud Abdulahusein wa bodi ya
michezo ya kubahatisha Mteja
wa benki ya Barclays Upendo John Lotuno akiokota moja ya kura za wateja
wakati wa kuchezesha bahati nasibi hiyo jana kutoka kushoto ni Rahma
Ngassa Meneja wa kitengo cha masoko Humud Abdulahusein na Tunu Kavishe
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano.
Modibo
Coulibaly mteja wa benki ya Barclays akimkabidhi Tunu Kavishe moja ya
kura za wateja wa benki hiyo ili kutangaza jina la mshindi wakati wa
kuchezesha bahati nasibu ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase,
kushoto ni Rahma Ngassa Meneja Masoko, wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa kitengo cha bidhaa Bwana.Samwel Mkuyu na Humud Abdulahusein wa bodi ya michezo ya kubahatisha
………………………………………………………………
Barclays Tanzania jana
imefanya droo yake ya kwanza ya kampeni ya Maisha Bomba na Barclays
Golden Briefcase kwa wateja wake muhimu wa sasa na wale wanaolengwa kwabaadaye.
Barclays jana imewapata washindi wake wa mwezi wa kwanza katika draw iliyofanyika katika ofisi zake hapa jijini dar es salaam.
Washindi hao 13 ni Erick
Mahenge and Anna Erick Mahenge, Khalid and Taeko, Mr.Severin Rweba
Celestin, Rashidi Saleh and Mr.Hemedi Ahmed, Mr.Saleh Koba Pili,
Mrs.Sheika Nasosr Salim, Mr.Hamid Khamis Othman, Mr.Arnold Rodrick
Shirima, Mr.Jamal AA and Mr.Kaushal HJ, Mr.Jack Fales Kamata,
Mr.Emmanuel Bernard Tungu, Mr.Pankaj Singh and Mr.Abdallah Rashid
Khamis.
Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu
wa kitengo cha bidhaa Bwana.Samwel Mkuyu alisema, “Barclays ilizindua
kampeni hii muhimu kwa wateja wao mwezi uliopita ambayo itawapa wateja
wao muhimu fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa muda wa
miezi mitatu (3)”.
Bwana Mkuyu
aliongeza na kusema kuwa “ukiweka pesa yako benki na ukaweza kubakisha
salio lililokusudiwa wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule
mpya ataweza kuingia kwenye droo ambapo wateja 13 watajinyakulia zawadi
mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya tshs millioni
kumi (10,000,000 TZS)” mwisho wa kampeni. Promosheni hii ilizinduliwa
rasmi tarehe11th April 2013 na itaendelea mpaka 30th June 2013.
Shindano hili liko wazi kwa
wateja binafsi, wapya na wa zamani, ambao wanaweka fedha zao na benki
yetu hapa Tanzania. Wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni
hii ni wale tu wenye account ya hundi (Current Account) au amana
(Savings), na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye account kwa shillingi
laki tano za kitanzania (500,000 tzs)au zaidi, na salio hili libakie
kwenye account hadi mwisho wa mwezi bila kupungua, Kila ongezeko la
shillingi Laki tano linampatia mteja ingizo la ziada katika katika droo
ya mwezi husika..
Zawadi
kubwa ya shilling million kumi za Kitanzania (shs. 10,000,000)
itatolewa mwisho wa kampeni. Zawadi zote zitawekwa kwenye Barclays
Golden Briefcase ambapo kila mshindi atatakiwa kuchagua mojawapo kisha
kuifungua ili kujua alichojishindia. Zawadi zinazoshindaniwa kila mwezi
ni iPads 2, vocha 8 za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya
shillingi laki 2 kila mmoja (TZS200, 000), mashine za kuoshea nguo 2, na
home theatre 1.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)