BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI (NEEC) KWA KUSHIRIKIANA NA KITUO CHA ELIMU YA BISHARA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDEC) KUWAPATIA MAFUNZO WANAFUNZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI (NEEC) KWA KUSHIRIKIANA NA KITUO CHA ELIMU YA BISHARA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDEC) KUWAPATIA MAFUNZO WANAFUNZI

Picha na 1Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Annacleti Kashuliza akifungua mafunzo ya wiki 3 ya Vijana 40 waliohitimu masomo ya elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana kazi leo jijini Dar es salaam .Mafunzo hayo kwa vijana yanalenga  kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi ya maendeleo na kuwafanya waweze kuajiri vijana wengine pamoja na kusaidiwa kupata fedha benki kwa ajili ya kuanzisha biashara kutokana na michanganuo watakayoiwasilisha.
Picha na 2Sehemu ya Vijana 40 waliohitimu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa  kuajiri vijana wengine. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Biashara yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) na Kituo cha  masuala ya Biashara na uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDEC) ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa vyuo vikuu nchini.
Picha na 3Sehemu ya Vijana 40 waliohitimu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa  kuajiri vijana wengine. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Biashara yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) na Kituo cha  masuala ya Biashara na uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDEC) ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa vyuo vikuu nchini.  Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages