ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO

Na Mwandishi Wetu
 
ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.

Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.

Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.

Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.


“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.


Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo,  walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!


Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.


Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.


“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.


Source: GLOBAL PUBLISHER WEBSITE

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages