Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwasilisha Taarifa ya
Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na
mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa
Fedha 2013/2014 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) inayoongozwa na Mhe.
Edward N. Lowassa (Mb.) (kulia). Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi
Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Aprili, 2013.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia-mstari wa
kwanza), akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati
ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa. Wengine katika picha ni Bw. John Haule
(katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na Balozi Rajabu Gamaha (kushoto), Naibu Katibu Mkuu.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani).
Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Wakurugenzi wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).
Baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo
na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao kati
ya Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Wakurugenzi na Wajumbe wengine kutoka
Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani) wakati wa kikao
kati ya uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiani wa Kimataifa





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)