WAKATI
wananchi wakilalamika kupanda kwa nauli kuwa kumeongeza ugumu wa
maisha, Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Daladala, Sabri Mabrouk
amesema bado nauli hiyo ni kiduchu. Mabrouk aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, kuwa wananchi wanapaswa kutambuwa kuwa ugumu wa maisha haukuanza leo.
Alisema
hali hiyo haikusababishwa na kupanda kwa nauli bali ulikuwepo tangu
utawala wa awamu ya kwanza na utaendelea kuwepo katika tawala mbalimbali
zitakazokuja.
“Kwa
watu tulioishi katika maisha ya ugumu ugumu ni kisema hivyo wananielewa
lakini najua wapo ambao wamenufaika kutokana na kuwa na jamaa ambao
walikuwa viongozi katika serikali hao labda ndio wanaweza kushindwa
kujua ugumu wa maisha katika nchi hii.
“pia
wananchi wajue kila kitu kizuri kina gharama zake hivyo ili kuboresha
huduma zetu za usafiri ni lazima wananchi wakubali kuchangia kile
kinachostahili” .”alisema Mbrouk.
Akizungumzia
mfumo wa huduma ya usafirishaji jijini kuwa wa kapuni, Mabrouk, alisema
haukwepiki bali ni mhuhimu kwa wamiliki wa daladala kutumia fursa hiyo
kujiunga na kuanzisha kampuni.
Aliwataka
wamiliki wenzake kuacha kuwasikiliza baadhi ya watu wanaotaka
kuwapotosha kuwa mpango huo haulengi kuwanufaisha wao bali kuna wahusika
maalum.
Mabrouk
alisema mfumo huo umewalenga wamiliki wa daladala kwanza, endapo
watadharau basi fursa hiyo itakwenda kweli kwa wengine.
“Kutakuwa
na kampuni mbili kwa kuanzia zitakazo simamia huduma hiyo ya usafiri
moja yadi yake yakuweka magari itakuwa Jangwani na nyingine itakuwa
katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi”alisema Mbrouk.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)