Leo ilikuwa ni siku ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba ngazi ya
Mtaa ambapo Dar ilifanyika leo na huo ni sehemu mojawapo ya Wakaazi wa
Mtaa waliojitokeza kwenye uchaguzi huu ambao niliushuhudia na kushiriki
kikamilifu.
Mmojawapo wa Wagombea, Abdulhaman Kasim Ngamba akinadi sera zake ambapo
mwisho wa siku aliibuka mshindi wa kwanza wa jumla kwa kundi la vijana
na kwa washiriki wote.
Mgombea mwingine Marry Chilala akinadi sera zake kwa Wananchi ambapo
naye pia aliibuka mshindi wa pili wa ujumla na mshindi wa kwanza kwa
upande wa kundi la Wanawake.
Mgombea
mwingine Emmanuel John akinadi sera zake kwa umma ambapo naye pia
aliibuka mshindi wa pili kwa upande wa kundi la vijana na mshindi wa
tatu kwa makundi yote. Kijana yupo safi.
Mgombea Emmanuel John akipiga kura
Ulifika wakati wa zoezi zima la kuhesabu kura ukawadia
Hapa Emmanuel John akitangazwa Mshindi wa Mjumbe wa Baraza la Katiba
Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutokana na uamuzi wa kura za Wananchi.
Kuja jamaa alipanda jukwaani kuja kumpongeza Emmanuel John kwa ushindi alioupata.
Mtu wa watu, Emmanuel John akipongezwa na Wananchi kwa ushindi wa kishindo aliouvuna
Kadri muda ulivyozidi kusonga kila mdau alikuwa na hamu ya kupiga picha na Emmanuel John.
Wakazi waliojitoza kwenye zoezi zima la uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Katiba Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)