Wachezaji
wa timu ya Far Rabat, wakiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, leo tayari kuwakabili wapinzani wao, Azam Fc katika
mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya pili, unaotarajia kupigwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, jumamosi ya wiki hii.
AKIZUNGUMZA
na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Nahodha wa timu ya Far Rabat Bellakhdar
Younes, amesema kuwa timu yake ipo kamili na inauhakika wa kuifunga
Azam FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika
utakaochezwa uwanja wa Taifa jumamosi wiki hii.
“Timu
yetu ni nzuri na Azam pia ni wazuri kwani wana wachezaji waliopo kwenye
timu ya taifa hivyo tutahakikisha tunafunga mabao 2-0 ili iwe rahisi
wakija nyumbani”, alisema Younes.
Wachezaji
wa Far Rabat ambao wapo kwenye timu ya Taifa ya Morocco ni Hammal
Younes, Achchakir Abderrahim, Bellakhdar Younes, Saidi Salaheddine,
Aqqal Salaheddine na Youssef Kaddior.
Timu hiyo imewasili ikiwa na msafara wa watu 31 na umefikia kwenye hoteli ya Saphire iliyoko Kariakoo.
Baadhi
ya viongozi wa timu hiyo wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, baada ya kuwasili leo mchana. Picha na Lenzi ya Michezo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)