Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa kutoa tamko la pamoja kwa umma la Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa Huduma za Simu kuhusu
Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania ambapo amesema Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania ikishirikiana na makampuni ya Simu na vyombo vya
usalama imeanza kampeni endelevu yenye lengo la kuwabaini wote
wanaohusika na uvunjifu wa sheria ili kuwalinda watumiaji wema na jamii
kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na ustawi
wa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za
mkononi ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akielezea jinsi kampuni yake
ilivyojidhatiti katika kutoa huduma kwa wateja na kuhakikisha kila namba
ya simu inayotolewa na kampuni ya simu ya Tigo inasajiliwa kwa mujibu
wa kifungu cha 102 (1) cha Sheria ya mawasiliano ya Elektroniki na Posta
(EPOCA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wa tatu kushoto) akiwa
meza kuu na Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Kampuni yanayotoa huduma za
simu nchini.
Baadhi maafisa mbalimbali na wawakilishi wa makampuni yanayotoa huduma za simu nchini katika mkutano huo.
Sehemu ya wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini.
--
Na.Mwandishi wetu
Watumiaji, watoa huduma, wakala wa
makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwa ujumla wamekumbushwa kuwa
ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya simu ambayo
haijasajiliwa.
Akitoa tamko la pamoja kwa umma la
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa Huduma za Simu
kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma amesema ni kosa
la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya
shilingi laki 5 au kifungo cha miezi mitatu.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha
130 cha Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka
2010, mtu yeyote ambaye anauza au anatoa kwa namna yeyote ile namba
namba ya simu bila kuisajili anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni
faini ya shilingi 3,000,000 ai kifungo cha miezi 12 au vyote.
Aidha Prof. Nkoma amewashauri watumiaji
wa simu za mkononi na wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa ili
kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na
kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta nay a
Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)