Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja
Baada
ya kukwama kwa Muda Mrefu Kutokana na baadhi ya wadhamini kushindwa kutimiza ahadi
zao za udhamini hatimaye Bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania imehamishia
fainali hizi za Miss Utalii Tanzania 2012/13 mkoani Tanga badala ya Dar es
salaam ambazo zilikuwa zifanyike awali. Taratibu zote za fainali za Show ya
Taifa kufanyika Tanga zimekamilika ikiwemo kukamilisha sheria
ya ya uendeshaji wa Shughuli za
sanaa na Fainali za Urembo ambapo Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa
hatimae limetoa kibali kwa fainali hizo Kufanyia Tanga tarehe 11.05.2013. waandaaji wamewasilisha BASATA uthibitisho wa
Zawadi kwa Washindi, Pamoja na mikataba ya kulinda haki na wajibu wa waandaaji
na washiriki wa Fainali Hizo.
Hii
itakuwa ni Mara ya kwanza kwa Mkoa wa Tanga kuwa wenyeji wa Fainali za Taifa za
mashindano ya Urembo na ni mara ya pili kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania Kufanyikia Nje ya Dar es salaam baada ya Fainali za mwaka 2005
kufanyikia Mkoani Arusha.
Hii
ni Heshima na Fulsa ya pekee kwa Mkoa wa Tanga ya kuhidhilishia na kuutangazia
Ulimwengu vivutio vyake vya Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, na Miundo mbinu
kitaifa na kimataifa. Lakini pia hii ni Fulsa kwa Jiji la Tanga kuuthibitishia
Ulimwengu kuwa Jiji la Tanga linao uwezo wa kuwa wenyeji wa Tukio la Kitaifa.
kufanyika kwa Shindano hili Mkoani Tanga kutasaidia pia Kuhamasisha pia Kampeni
dhidiya , Uharibifu wa mazingira, Uvuvi Haramu, Uwindaji Haramu, Tohara kwa
wanawake, Utamaduni, mila na Desturi kongwe na Potofu.Madawa ya kulevya,
Rushwa, Ubaguzi wa Kijinsia, na Mmomonyoko wa Maadili katika jamii.
Wakati
huo serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewapongeza juhudi zinazo
fanywana Waandaaji wa Miss Utalii Tanzania
za kutangaza vivutio vya utalii na utamaduni wa Tanzania kitaifa na
kimataifa kwa kuipatia Sifa kubwa Tanzania kupitia mashindano hayo. Kwa mujibu
wa maelezo ya Barua ya Tarehe 19.04.2013 iliyo sainiwa na Ndugu Z. A Kimwaga
kwa niaba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kwa waandaaji
wa Miss Utalii Tanzania. Wizara na serikali kwa ujumla inatambua juhudi
zinazofanywa na waandaaji wa mashindano haya katika kukuza utalii wa ndani na
Utalii wa Kitamaduni.
Katika
kuthibitisha hilo Wizara imewashauri waandaaji wa mashindano hayo kuwaslisha
maoombi ya msaada kutoka serikalini kwa wakati na kwa kuzingatia misimu na
Bajeti ta serikali ili kuwe na uwezekano wa serikali Kudhamini mashindano hayo.
Hata hivyo Serikali kupitia Taasisi zake za Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa(TANAPA)
, Mamlaka ya Ngorongoro(NCIA), na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa miaka yote
ikiwepo mwaka huu imekuwa ikitoa udhamini wa Hali na Mali katika kufanikisha
Mashindano hayo.
Nae
Rais wa Mashindano hayo Gidion Chipungahelo kwa niaba ya Bodi ya Mashindano
amewaomba Radhi watanzania wote , wadau w ashindano , washiriki, wadhamini na
wengine wote walioguswa au kuathiriwa kwa namna yoyote
Washindi wa 1-5 wa Fainali
za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia
yakiwemo ya International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation,
Miss Heritage World, Miss Tourism University World, Miss Globe International
n.k
Miss Utalii Tanzania ,hadi
sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya
Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism
World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World
2008-Personality n.k
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)