NIMR YAANZA LEO MKUTANO WAKE 27 WA WANASAYANSI WATAFITI JIJINI ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

NIMR YAANZA LEO MKUTANO WAKE 27 WA WANASAYANSI WATAFITI JIJINI ARUSHA

 
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo imeanza mkutano wake wa 27 wa mwaka kwa watafiti Wanasayansi jijini Arusha ambapo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein anataraji kuufungua rasmi jioni ya leo.

Pamopoja na Mkutano huo wa NIMR, pia mkutano wa pili wa Wanasansi kuhusiana na Masuala ya Afya barani Afrika unafanyika sambamba na mkutano huo ambapo watafiti mbalimbali duniani wanatoa mada juu ya tafiti mbalimbali za magonjwa ya binadamu.

Mkutano huo ambao umebeba kauli Mbiu ya Mabadiliko ya Mazingira katika Utafiti wa Afya 'Changing landscape in Health Research' utafanyika kwa siku nne katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha.

Pichani ni Dk. Jeff Waage kutoka Uingereza akiwasilisha mada juu ya Kilimo na Afya katika Mabadiliko ya Mazigira katika Utafiti wa Afya.
Baadhi ya washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha hii leo. Baadhi ya Wabunge nao wamealikwa kushiriki katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages