Baada ya siku tano za hofu kuu kwa wakazi wa Boston, jimbo la
Massachusetts na vitongoji vyake, polisi walimkamata mshukiwa wa pili
kufuatia milipuko ya mabomu wakati wa mashindano ya riadha mjini humo
Jumatatu.
Mshukiwa huyo Dzhokhar Tsarnaev mwenye umri wa miaka 19 yumo chini ya ulinzi mkali wa polisi Jumamosi katika hospitali ya Beth Israel Deaconess Medical Center mjini Boston, ambapo yaripotiwa kuwa yuko katika hali mahtuti.
Kakake mwenye umri wa miaka 26 Tamerlan aliuawa katika makabiliano ya risasi na polisi Alhamis usiku huku Dzhokar akitoroka kwa mguu.
Baada ya msako mkali Ijumaa hatimaye polisi walimpata Tsarnaev akiwa amejificha kwenye boti nyuma ya nyumba moja katika kitongoji cha Watertown mjini Boston. Maafisa wanasema alijisalimisha baada ya kufyatuliana risasi na polisi.
Mara baada ya habari za kukamatwa kwake, wakaazi wa Boston walijitokeza mjini kusherehekea na kupongeza juhudi za polisi na wote waliohusika katika msako huo wakiwemo maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai FBI. Baada ya taarifa hizo rais wa Marekani Barack Obama aliwapongeza wote waliohusika na msako huo akisema juhudi zao ni dhahiri kuwa Marekani imekataa kuhangaishwa na magaidi.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)