Mchakato wa kumsaka Redd’ Miss Tanzania waaza rasmi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Mchakato wa kumsaka Redd’ Miss Tanzania waaza rasmi



Warembo watakaowania taji la Redd's Miss Dar Indian Ocean wakimsikiliza kwa Umakini Mkurygenzi Mkuu wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga wakati alipowatembelea warembo hao kwenye kambi yao ya Mazoezi.Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye.

HATUA za awali za kumsaka Redd’s Miss Tanzania sasa zinaanza kushika kasi, wakati wiki hii kutakapokuwa na kinyang’anyiro katika vitongoji kadhaa vya kusaka warembo wao.

Kazi kubwa itaanza Morogoro, wakati atakaposakwa Redd’s Miss High Learning atakayeuwakilisha mkoa huo katika kumpata mrembo kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu, shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Sirvoy
Wakati Morogoro Miss High Learning akipatikana kesho, shughuli pevu ipo keshokutwa (Jumamosi) pale kutakapokuwa na shindano la kumsaka Redd’s Miss UDOM, litakalofanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma
Siku hiyo pia atapatikana mwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Kagera na Mwanza, shindano ambalo litafanyika Yacht Club, Mwanza.

Akizungumzia kuhusu Redd’s Miss Morogoro High Learning, mratibu wa shindano hilo, Verdian Kamugisha alisema kila kitu kimekamilika na kutakuwa na burudani za kufa mtu.

“Tumekamilisha kila kitu na warembo wote wako katika hali nzuri na kutakuwa na burudani za kumwaga, wakazi wa Morogo wanatakiwa kuja kwa wingi kushuhudia kile kitakachotukia,” alisema.

Mratibu wa Shindano la Redd’s Miss UDOM, Rachel Matina naye alisema kila kitu kwao kipo tayari na watu wanatakiwa kufika kwa wingi kushuhudia jinsi warembo kutoka Chuo Kikuu Dodoma, walivyopania kulitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania mwaka huu.

Joseph Rwebangira wa anayeratibu shindano la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mikoa ya Kagera na Mwanza naye alikiri kukamilika kwa maandalizi yote na kutakuwa na burudani za kila aina siku ya onyesho.

Upande wa kanda ya kaskazini mwa nchi kutakuwa na shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Hai ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Snow View na mkoani Mara katika kitongoji cha Tarime shindano litakuwa katika ukumbi wa JJ Club na maandalizi kwa sehemu zote husika yameshakamilika kwa kiwango kikubwa.

Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages