Kamishina jenerali wa jeshi la magereza,
John Casmir Minja akikagua gwaride la heshima kabla ya kuwatunukia
askari wa jeshi hilo 21, kanda ya kusini.
Picha juu na chini ni Kamishina
jenerali wa jeshi la magereza, John Casmir Minja akiwatunuku nishani
maofisa 21 wa jeshi la magereza kanda ya kusini
Maofisa Watunukiwa wakisubiru kupata nishani zao.
Kamishina jenerali wa jeshi la magereza, John Casmir Minja akiwa na Akiwa na viongozi wa Wilaya na Mkoa.
Kamishina jenerali akiwa na maafisa wa ngazi za juu wa jeshilo hilo katika picha ya pamoja.
Kamishina katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani kanda ya kusini.Picha zote na Godwin Msalichuma
--
Askari 21 wa jeshi la magereza kanda ya
kusini, wametunukiwa nishati za heshima na kamishina jenerali wa jeshi
hilo, John Casmir Minja, kwa niaba ya amiri jeshi mkuu wa majeshi nchini
Rais, Dkt, Jakaya
Kikwete, katika gereza la Lilungu mjini Mtwara.
Kikwete, katika gereza la Lilungu mjini Mtwara.
Nishati hizo zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni ya utumishi uliotukuka, ya mwenge wa uhuru na ya Utumishi wa muda mrefu, ambapo nishani ya Utumishi uliotukuka hupewa askar ambaye ametumikia kwa miaka 20 mfululizo, ya mwenge wa uhuru ni yule ambaye alizaliwa wakati nchi yetu inapata uhuru na ametumikia kwa miaka 35 mfululizo na ya Utumishi wa muda mrefu hupewa yule aliyetumikia kwa miaka 15
mfululizo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)