Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama
Asha Suleiman Iddi akimkabidhi Bwana Zaid Omar Nahoda Shilingi Milioni
tatu{3,000,000/-} zilizotolewa na Balozi Seif kama
fidia ya nyumba yake baada ya kuridhia eneo ilipo nyumba yake litumike
kwa shughuli za maendeleo ya majengo ya Skuli ya Msingi Mgambo.
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama
Asha Suleiman Iddi akimkabidhi Bwana Zaid Omar Nahoda Shilingi Milioni
tatu{3,000,000/-}zilizotolewa na Balozi Seif kama
fidia ya nyumba yake baada ya kuridhia eneo ilipo nyumba yake litumike
kwa shughuli za maendeleo ya majengo ya Skuli ya Msingi Mgambo.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
--
Kamati
za maskuli katika maeneo yenye upungufu wa madarasa Nchini zimehimizwa
kuwashajiisha wananchi wa maeneo yao kujikita zaidi katika ushirikiano
wa kukabiliana na changa moto hizo ili kuwapa fursa nzuri watoto wao wa
kusoma kwa utulivu.
Mke wa
Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi alitoa himizo hilo
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Shilingi Milioni 3,000,000/-
zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya
kulipwa fidia Bwana Zaid Omar Nahoda aliyejitolea kubomoa nyumba yake
kupisha eneo hilo kutumiwa kwa maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Skuli
ya Mgambo.
Makabidhiano
hayo yaliyoshuhudiwa pia na Uongozi wa Serikali na CCM Wilaya ya
Kaskazini B, Kamati ya Skuli,Wazazi pamoja na Wananfunzi imefanyika
katika Skuli ya Msingi ya Mgambo iliyomo ndani ya Jimbo la Kitope Wilaya
ya Kaskazini B.
Mama
Asha alisema kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliopo
Duniani hivi sasa Wazazi wanapaswa kuwajengea mazingira yanayolingana na
mabadiliko hayo watoto wao ili wasome kwa uhakika katika kukabiliana na
changamoto zilizowazunguuka.
Aliwaasa
wanafunzi wa skuli hiyo kuonyesha jitihada zao katika masomo yao
wakielewa kwamba suala la elimu ni la lazima sambamba na kuwapa faraja
wazazi wao.
Akizungumzia
tatizo kubwa na ajali za bara barani kutokana na mwendo wa kasi
unaofanywa na baadhi ya madereva wanaotumia bara bara iendayo kaskazini
Mama Asha aliziomba Halmashauri za Wilaya za Kaskazini A na B
kushirikiana pamoja katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Alisema
baadhi ya madereva hao wanasahau kwamba bara bara hutumiwa na watu wote
waliwemo watoto na walemavu. Hivyo ipo haja kwa taasisi zinazohusika
kuzitupia macho sheria za usalama bara barani ili ziweze kuongezewa
nguvu zaidi.
Mapema
akitoa taarifa ya Skuli hiyo Mwalimu Mkuu msaidizi wa Skuli ya Mgambo
Ndugu Salim Seif alisema skuli hiyo bado inaendelea kukabiliwa na changa
moto kadhaa ikiwemo Ukosefu wa Maabara, walimu wa sayansi pamoja na
utanuzi wa majengo ya skuli kwa lengo la kukabiliana na ufinyu wa
madarasa.
Wakati
huo huo Mke wa Mbunge wa Jimbo hilo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi
alikabidhi Vifaa mbali mbali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo
cha Elimu ya Maandalizi cha Dhin Noorayn kilichopo katika Kijiji cha
Fujoni.
Akikabidhi
Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi
kutimiza ahadi aliyoitoa kwa uongozi wa Kituo hicho wakati wa ziara yake
Mama Asha aliwaomba wazazi kujitahidi kuchangia vituo hivyo ili kuwapa
moyo walimu wanao wahudumia watoto wao.
Mama
Asha alifahamisha kwa vituo vya maandalizi mara nyingi vimekuwa
vikisaidia kutoa fursa kwa wazazi kusaidiwa ulezi hali inayowapa muda
wa kujikita zaidi katika harakati zao za kiuchumi na maendeleo.
Mapema
Mwalimu Mkuu msadizi wa Kituo hicho cha Dhin Noorayn Bibi Hawana
Abdulla kwa niaba ya uongozi na walimu wa kituo hicho wameelezea faraja
yao kutokana na ushirikiano wanaoupata wa uendelezaji wa kituo hicho.
Vifaa
hivyo vya ujenzi ambavyo ni pamoja na Bati, misumari, mbao, miti,
matofali, mchanga vimegharimu zaidi ya shilingi milioni 4.9.
Na
Khamis Ame,
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)