JE SABABU HIZI ZA WANAWAKE ZINA UKWELI:SABABU KUU ZA WANAWAKE WENGI KUVAA NGUO ZA NUSU UCHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

JE SABABU HIZI ZA WANAWAKE ZINA UKWELI:SABABU KUU ZA WANAWAKE WENGI KUVAA NGUO ZA NUSU UCHI

Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.
 
 Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo. 
 
Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao.Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.
 
 Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.
Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. 
 
Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa. 
 
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. 
 
Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo. 

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages