bondia kamandawamakanda kushoto akitunishiana misuli na ibrahim maokola baada ya kusaini pambano lao
bingwa wa kike na msaidizi wa promota pendo njau akisimamia zoezi la
usainishaji wa mikataba ya mabondia,likiwemo pambano la kuondoa utata
kati ya kamanda na maokola,.bigright jafet kaseba na mabondia wengi
walishuhudia
Bondia jafet kaseba anategema kupanda tena ulingoni mwanzoni mwa mwezi
wa sita kuzipiga na bondia toka kenya joseph magudha katika mpambano wa
kimataifa. hivyo maandalizi yamekwishaanza kwa kuwaanda mabondia
watakaocheza utangulizi,kwa kuweka mapambano makali likiwemo la kamanda
wa makamanda atakaezipiga na ibrahim maokola. mwanzoni maokola alikuwa
amepangwa azipige na bondia toka moro na kamanda kupewa bondia mwingine,
lakini kulitokea kupishana kwa maneno kati ya mabondia hao kiasi cha
kutaka kupigana kavu, mabondia na viongozi waliokuwepo hapo akiwemo
ibrahim kamwe walipendekeza ibadilishwe wapinzani na wawili hao wazipige
kukata ngebe na majigambo ya ubabe waliyokuwa wakitupiana.mpaka sasa
mapambano ya utangulizi inategemea kuwa juma seleman atazipiga na issa
omar,juma fundi atapigana na moro best, yohana mathayo atazipiga joseph
onyango toka kenya. na mapambano mengine yatajulishwa hapo baadae zoezi
la usainishaji mikataba likikamilika
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)