Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga


Masanii  maarufu kwa vichekesho Masele  wa kundi la vituko shoo toka Dar es salaam akitoa burudani kwa wakazi wa Tanga  wakati wa Tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga
Umati wa wakazi wa Tanga wamejitokeza kushuhudia burudani na kuzindua rasmi huduma ya Airtel yatosha mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano mkoani humo
Wasanii wa kundi la Toto afrika wakionyesha umahiri wao wa kucheza na moto jukwaani wakati wa tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya tangamano mkoani tanga mwishoni mwa wiki 
Masanii Erick wa kundi vituko shoo toka Dar es salaam akitoa burudani kwa wakati wa Tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel ya Airtel yatosha katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga
Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na utaratibu wake wa
kufanya matamasha ya wazi yenye lengo la kutoa burudani pamoja na
kuitambulisha huduma yake mpya ya AIRTEL YATOSHA kwa jamii ambapo
mwishoni mwa hii Airtel ilifanya tamasha katika viwanja vya Tangamano
mjini hapo.

 Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema "Airtel tumefurahishwa sana na umati wananchi wanaojitokeza kwaajili ya burudani lakini pia inatusaidia kuwajulisha
wote habari njema za unafuu wa gharama za mawasiliano kupitia huduma
yetu ya Airtel YATOSHA Tunawakumbusha kuwa YATOSHA ni huduma ya kudumu na inasaidia sana kupunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wetu. 

Kujiunga na huduma hii ili ujipatie vifurushi vya SIKU au WIKI piga *149*99# "Binafsi nimeshangaa na kufurahi sana sana kwa uwepo wa kifushi cha TOSHA cha hadi shilingi 349" na najipatia dakika 25 kuongea bure du
kweli hii Imetosha!" alisikika akisema Hassan Juma mkazi wa chumba
geni mkoani Tanga mara baada ya uzinduzi huo wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwemo Ney wa Nitego, Nadii, Fid Q, na Juma Nature akiwa na kundi lake walipanda jukwaani kutoa burudani mfululizo huku wananchi
waliojitokeza wakifuatia burudani hiyo mwanzo mwisho Kati ya vibao vilivyopigwa na wasanii hao na kuwavutia wakazi wa Tanga ni pamoja na kile cha 'nani kwamwaga pombe yangu kilichoimbwa na Madee
toka kundi la Tip Top Connection, wakati wahudhuriaji wa tamasha hilo
wengi wao walionekana kuvutiwa zaidi na msanii wa hip hop Ney wa
mitego hasa kwa umahiri wake wa kupanga mistari na free style zake
alipoachia free style. 
 
Airtel inaendelea kufanya uzinduzi wa huduma ya airtel yatosha
kupitia matamasha ya burudani kwa ambapo baada ya tamasha la Dar es
salaam, Morogoro, Chalinze na Tanga kupita airtel yatosha jumamosi na
jumapili hii inahamia jijini Mwanza katika viwanja vya Furaisha ambapo
wasanii wa bongo flava watatoa burudani bure

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages