Mwili
wa marehemu, Romanus Masige mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro ukiwa
umelala chini katika barabara ya Old Dar es Salaam eneo la maktaba ya
mkoa wa Morogoro baada ya kudaiwa kusukumwa na wenzake waliokuwa nao
wamepakiwa nyuma ya lori wakati wakisafiri kutoka Kihonda kuelekea kituo
kikuu cha polisi mjini hapa.
Shuhuda akieleza tukio zima lililotokea
Mwili wa marhemu Masige ukiwa umefunikwa kwenye eneo la tukio
Mwili wa marehemu ukipelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi
Hili gali ndilo lililomkanyaga marehemu
Msamalia akimwaga mchanga kwenye damu ya mtu aliyekanygwa na gari .Picha na Jackson Audiface
.......................
Msamalia akimwaga mchanga kwenye damu ya mtu aliyekanygwa na gari .Picha na Jackson Audiface
.......................
Mashuhuda
ambao walishuhudia tukio hilo walitudokeza kuwa nyuma ya
lori hilo ilikuwa imebeba kokoto na abiria wawili na mara baada ya kufika
eneo hilo alionekana moja wao akimsukuma marehemu aliyedondoka chini na
gurudumu la nyuma lilimkanyaga na kupoteza maisha papo hapo huku
mwenzake baada ya gari kusimama alichukua baiskeli na kutoweka eneo la tukio
wakati dereva akijisalimisha kituo cha polisi.
"Alikanyagwa
kichwani huyu marehemu na hilo lori baada ya kusukumwa na mwenzake na
gari iliposimama alichukua baiskeli na kutoweka eneo hilo
hatukuweza kuelewa nini kinaendelea". Kilisema Chanzo chetu.
Habari
hizi kupitia blog hii iliendelea kudokezwa kuwa mkasa huo kwa marehemu
huyo ulitokana na kitendo chake cha kupinga bosi wake kuuziwa kokoto hizo
mara mbili jambo ambalo hakukubaliana nalo na kuwaona wahusika
waliopeleka kokoto hizo kuwashuku kuwa ni wezi ndipo safari ya
kuwapeleka kituo kikuu cha polisi na kabla hawajafika kituoni tukio hilo
likatokea majira ya saa 10 jioni jana.
Marehemu Masige
ni mkazi wa Kihonda akiwa ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma ambapo taarifa
zilizotufikia punde zinasema kuwa mwili wa marehemu huyo utasafirishwa
kwa ajili ya mazishi mkoani Kigoma.
Masige alikuwa Mwalimu wa kwaya katika kanisa katoliki kigango cha kristo mfalme na mlinzi katika kanisa hilo.
Mungu ailaze mahala pema peponi Amina
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)