Zijue Sababu Zinazomtoa Mwanamke Nje ya Ndoa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Zijue Sababu Zinazomtoa Mwanamke Nje ya Ndoa

JAPOKUWA wanawake bado hawajapita wanaume katika suala la kutoka nje ya ndoa, idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa na kutafuta mabwana wengine ili kuwatimizia haja yao ya tendo la ndo imeongezeka, kwa hapa nyumbani inasemekana kati ya asilimia 14-16 ya wanawake walio kwenye ndoa wameshalala na wanaume wengine takribani mara moja katika maisha yao ya ndoa. Wanaume wapo juu kidogo, kati ya asilimia 20-30, wameshatoka na wanawake wengine, wengi wao wakiwa ni wanawake ambao wanafanya nao kazi au marafiki wa karibu. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayosababisha wanawake watike nje ya ndoa.

1. Uhaba wa tendo la ndoa.
Unakumbuka wakati mnaanza kutongozana na kuchumbiana, meseji na simu haziishi bebi nakupenda bebi sijui nini. Ghafla watoto anapata mimba, watoto wanazaliwa, majukumu yanaongezeka, kazi zinazidi. Ukirudi nyumbani wewe ni kula kuoga na kulala, unasahau kwamba wanawake siku zote wanataka wajione wanatakwa, kama unajifanya humtaki na humuonyeshi kama yeye ni mzuri, ataenda kutafuta mtu ambaye anamuonyesha kwamba anamtaka. Achana na mambo ya kujifanya mtu mzima, mbusu mke wako hadharani, mshike mkoni, mtumie meseji za uchokozi. Ukifanya hivyo utajikuta damu bado inachemka na bado mnatakana hata kama mna miaka 70.

2. Kuonyesha utundu.
Asikudanganye mtu kila msichana ana utundu wake ambao ameuficha mahali anasubiri uuvumbue. Kama anajifanya mwanamke wa heshima, mnazima taa ndio mnaendelea na mambo yenu, anajifanya anaona aibu na wewe unamuamini hivyo hivyo. Ni kazi yako wewe mwanaume kuutafuta utundu wa mkeo uko wapi, mfanye awe huru kufanya jambo analotaka kufanya na wewe na wala usimjaji kwamba amejifunzia wapi. Usipofanya hivyo ataenda kumtafuta jamaa ambaye atamfanya awe huru kuonyesha utaalamu wake (inner sex kitten)

3. Kujithamini (Self-esteem)
Tendo la ndo linamfanya mwanamke ajithamini zaidi, ajione mrembo na kwamaba anapendwa. Kama mke au demu wako anaonyesha kutojithamini na kwambwa wewe utakuwa unatamani au unapenda kulala na wasichana wazuri kuliko yeye, ni kazi yako kumfanya ajisikie mzuri, ajithamini nakujipenda zaidi. Usipofanya hivyo kuna jamaa huko nje ataropoka, duh! leo umependeza na mambo yanaweza kuishia pengine.

4. Kulipiza kisasi
Hapana, sio kulipiza kisasi kwasababu amekukamata kwamba umelala na mwanamke mwingine, wanawake wanaweza kuona kuwa namna ya kukuumiza ni kwenda kulala na mwanaume mwingine kwa kulipiza kisasi kwa kosa ulilofanya, iwe ni kwamba ulikamatwa ukidanganya, umemuumiza moyo wake, na anapunguza uaminifu kwako na kutojali kukuumiza wewe. Ili kurudisha uaminifu, haitoshi kumwambia tu kwama samahani, na matendo yako yanatakiwa yabadilike.

Jaribu kuzingatia mambo haya na utaondoa vishawishi vya kusababisha mke wako aende kutimiza haja yake ya tendo la ndoa na mwanaume mwingine. Imeandaliwa na http://www.thehabari.com/.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages