Mgeni
rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na
wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani
walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika
hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos
inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine
amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya
biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa
serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.
Afisa
Mauzo wa kampuni ya Alliance Autors Julius Guni akizungumza na vyombo
vya habari akisema kuwa kampuni hiyo imeweza kutambulisha magari mapya
aina ya Volkswagon amboyo yamefanyiwa ‘engineering’ ya Kijerumani hivyo
ni magari madhubuti sana. Aidha
amesema kupitia Chama cha Wauza Magari (TMTA) tunaitaka serikali
kuhakikisha inaangalia sana suala la ushuru ili kila mtu aweze kuwa na
uwezo wa kumiliki gari, hivyo tukishirikiana na makampuni mengine
yanayouza magari kupambana tuweze kupata unafuu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (kulia) akiongozana na
Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya
Ujerumani (kushoto) baada ya kuupokea Ujumbe kutoka nchini Ujerumani
kunakotengenezwa magari aina ya Volks Wagon walipofika kushuhudia
uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari
ya Volkswagon. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mh. Klaus
Peter Brandes aliyeambata na ugeni huo.
Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya
Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya Kampuni ya
Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro akipokea
wageni waalikwa.
Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp(kulia) wakifurahia hotuba ya Dkt.
Mwakyembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza wakati
wa uzinduzi huo ambapo amesema kufuatia kupanuka kwa kampuni ya
Alliance Autos na kuongezeka kwa wateja tumeonelea ni vizuri kufungua
showroom mpya ya magari ya Volkswagon ambapo wateja wanaweza kuitembelea
wakati wowote.
Mgeni
rasmi Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia)
akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy
Sharp (hayupo pichani) akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa
Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos
(T) LTD. Kulia ni Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya
Uchumi na Teknolojia wa Ujerumani. Kushoto ni Tender Manager wa CFAO
Motors Bw. Marco Kahabi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa
Ujerumani, Prof. Harald Braun (wa pili kushoto).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun
akizungumza machache na wageni waalikwa ambapo amesema ziara ya Ujumbe
kutoka Ujerumani imekuwa na mafanikio si tu kwa mazungumzo na Serikali
bali kwa kufanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa Showroom mpya ya magari ya
Volkswagon ya kampuni ya Alliance Autos na kupata fursa ya kubadilishana
mawazo na wafanyabiashara watanzania.
Bw.
Lionel Roux wa CFAO Paris Ufaransa akitoa salamu kwa wageni waalikwa
wakati wa ufunguzi wa Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya
Kampuni ya Alliance Autos.
Meneja
Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja
(kushoto), Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius
Guni (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof.
Harald Braun(hayupo pichani).
Johns Wiseman wa Volkswagon Group katika uzinduzi huo.
Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi (kulia) akiteta jambo na
Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Makyembe. Wa pili kulia ni
Balozi wa Ujerumani nchini Mh.Klaus Peter Brandes.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni na
mmoja wa wageni waalikwa wakikagua magari mapya aina ya Volkswagon ya
Kampuni ya Alliance Autos kwenye showroom mpya iliyozinduliwa jana
jijini Dar na Waziri wa Uchukuzi Dr. Mwakyembe.
Mkurugenzi
Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha akipata maelezo ya gari aina
ya Volkswagon TIGUAN kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance
Autos (T) LTD Bw. Julius Guni wakati wa hafla ya uzinduzi wa showroom
hiyo.
Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kulia) na Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni (katikati) wakibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Picha
juu na chini ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp
akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa showroom
mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos jijini
Dar.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakinywa na kufurahi baada wakati wa uzinduzi wa
Show room mpya ya Kampuni ya magari aina ya Volkswagon ya Alliance Autos
jijini Dar.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja waliohudhuria uzinduzi huo.
Picha
juu na chini ni Wakwetu Band ikiongozwa na Carola Kinasha kutoa
burudani kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa showroom mpya na ya
kisasa ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani na Ujumbe wake.
Afisa Mauzo wa Alliance Autos David Kritsos (katikati) na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Operations Manager wa Golden Tulip Bw. Aatish Ladwa(kushoto) na mmoja wa wageni waalikwa.
Warembo
wa Volkswagon waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye hafla ya uzinduzi
wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos iliyopo maeneo ya
Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)