Jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV za jijini Dar Es
Salaam,kwa staili ya GUINNESS® FOOTBALL
CHALLENGE™, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Tanzania walioonesha
kwamba hakuna kisichoshindikana na
hakuna kufa moyo kabisa katika mchezo huu ambao sasa hivi unatazamwa na wengi
barani Afrika.
Wawili hao waliishia kwenye sare kwa raundi mbili na kuthubutu
kuingia kwenye nusu fainali ambapo wana
nafasi ya kupandisha kitita chao hadi dola za kimarekani 5,500 (USD 5500) kwenye ukuta wa pesa wa Guinness.
Daniel
na Mwalimu walionesha umuhimu wa kutokata tamaa na sasa wameingia kwa kishindo
kikubwa kuwakilisha Tanzania kupambana na nchi zingine za Afrika. Kwenye raundi hii ya kucheza na nchi zingine
zilizokuwa kwenye jumuiya ya Afrika mashariki, ikumbukwe kuwa kuna dola za kimarekani 250,000 ($250,000) za
kushindaniwa .
Wiki
ijayo tutaweza kuona timu zingine nne kutoka hapa hapa Afrika mashariki
zikichuana vikali na kuonesha umahiri wao, Je wataweza kuingia na kuwakilisha nchi zao kupambana na nchi zingine za
Afrika? Je timu nyingine kutoka Tanzania
itaweza kuwapiga chini wakenya na waganda ili tuwe na timu mbili kwenye raundi
ya ‘Pan Africa ’?
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga
kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Kipindi hiki kuanzia
jana kitakua kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV,
kwa ITV itakua ni saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku na saa mbili na dakika kumi na tano(2:15)
usiku Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guinness wakati ukitazama kipindi hiki.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)