Meneja wa
QX,Ally Abdalah (kulia) na Mpishi Mkuu wa Bar hiyo, Emanuel Seneyo (wa pili kushoto)
wakionyesha kitita cha shilingi milioni moja baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munasa(wa pili kushoto) ikiwa ni mabingwa wa Safari Nyama Choma Mkoa wa Arusha yalifanyika
katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.Wa pili kulia ni Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo,Meneja Mauzo wa Kanda, Kitio Wilderson na
mhudumu wa Bar ya QX akishangilia kwa furaha.
Meneja wa
QX,Ally Abdalah(kulia) na Mpishi Mkuu wa Bar hiyo, Emanuel Seneyo(wa pili
kushoto) wakionyesha kitita cha shilingi milioni moja baada ya kukabidhiwa na
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munasa(kushoto) ikiwa ni mabingwa wa Safari Nyama Choma Mkoa wa Arusha yalifanyika
katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.Wa pili kulia ni Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja Mauzo wa Kanda, Kitio Wilderson.
Mashabiki wa
Bar ya QX ya Arusha wakishangilia na Meneja, Ally Abdalah (wa pili kulia) mara
baada ya kutangazwa mabingwa wa Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha
yaliyofanyika katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
QX Pub, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma
Mkoa wa Aresha, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano
hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari
Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika
juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa General Tyre, baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim
Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani
hapa, Royal Stop Over Pub, walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha
Sh 800,000 na cheti, wakati Blue Line Pub walishika nafasi ya tatu na kupata
zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya Rombo Delux
iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya VIP Longe ilishika nafasi ya
tano na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa
fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo
juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni
usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi,
uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini
wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL
na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani hapa kabla
ya kuhamia mkoa wa Moshi na wa mwisho.
“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa
zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Arusha
tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama
hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate
nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36
na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo
ndio inayoongoza kwa mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Arumeru, NyerembeMunasa, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa
mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika
kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool
Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo mbalimbali
kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa
nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,”
alisema.
Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa
na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha
yale waliyokosea mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)