WAKAZI ZAIDI YA 160,000 JIJINI MWANZA KUNUFAIKA KWA MRADI WA MAJI KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI(SBL) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAKAZI ZAIDI YA 160,000 JIJINI MWANZA KUNUFAIKA KWA MRADI WA MAJI KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI(SBL)





Mke wa rais mama Salma Kikwete akisaidiana na Meneja miradi wa SBL Nandi Mwiyombela wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji la Mwanza Getrude Ngonyani kuashiria kuanza kutumika kwa kisima kwa ajili ya wakazi wa Mwanza.



 Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa ajili ya wakazi zaidi ya 160,000 waishio jijini Mwanza, kushoto kwake ni  Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Pascal K. Mabiti na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Jaji Mark Bomani.
Meneja miradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL) Nandi Mwiyombela
akitoa maelezo kwa mke wa Rais mama Salma Kikwetejuu ya kisima
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti katika Hospitali ya mkoa wa Mwanza - Sekou Toure.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akihutubia wakazi wa jiji la Mwanza(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti katika eneo la  hospitali ya Sekou Toure ulifanyika Alhamisi ya wiki hii.
Meneja miradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela katikati akisalimiana na mke wa rais mama Salma Kikwete mara baada yakuwasili katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwaajili ya uzinduzi wa kisima cha maji na pembeni yake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mwanza Patrick Kisaka.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages