RAIS KIKWETE AMTEMBELEA MZEE YUSUF MZIMBA ALIYELAZWA MUHIMBILI KWA KUGONGWA NA BODABODA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA MZEE YUSUF MZIMBA ALIYELAZWA MUHIMBILI KWA KUGONGWA NA BODABODA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee` Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans (YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka.PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages