Raisi
wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo wa Kwanza Kushoto,
Kaimu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Muheshimiwa Songolo
pamoja na Ndugu Adam Chipungahelo, wakati walipofika katika Ofisi yake.
Raisi wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akizungumza Jambo
Muheshimiwa Songolo Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni , akizungumza jambo
Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Muheshimiwa Songolo akiwa anafuatilia kwa umakini kikao.
Kamati
ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania Ikiongozwa na Rais wa Mashindano
hayo Ndugu Erasto G. Chipungahelo Jana Tarehe 12.03.2013 Ndugu.....
katika ofisi yake iliyopo Kinondoni Manispaa Jijini Dar es salaam Akiwa
ameambatana na Baadhi ya Viongozi wa Kamati hiyo ambaye ni Ndugu Adam
Chipungahelo ambaye ni Mratibu wa Matukio Miss Utalii Tanzania na Bwana
Fredy Njeje ambaye ni Meneja wa Masoko na mahusiano Miss Utalii
Tanzania, Ndugu Chipugahelo Alimshukuru Naibu Mustahiki Meya kwa
mapokezi na ushirikiano wanayo pata kutoka kwa Manispaa hiyo ambapo
warembo wapo kambini katika Hoteli ya Ikondolelo Lodge iliyopo Kibamba
Manispaa ya Kinondoni. Amemuhakikishia Naibu Meya Kuwa Miss Utalii
Tanzania Imejipanga kutangaza Utalii, Utamaduni na Mianya ya uwekezaji
Manispaa ya Kinondoni kitaifa na Kimataifa ili hatimaye Kinondoni iwe
kati ya Wilaya nchini.
Akizungumza
katika Kikao Hicho Naibu Mustahiki Meya Aliwashukuru waandaaji wa
Mashindano Hayo kwa Kuteuwa Manispaa ya Kinondoni kuwa makazi ya warembo
wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13. Hii ni Fulsa pekee kwa Manispaa
yetu kimataifa na Kimataifa lakini pia ni Fulsa kwa Manispaa ya
Kinondoni kuuthibitishia Ulimwengu kuwa Tunavivutio vingi vya utalii
kuanzia mahoteli, Maeneo ya kihistoria
,
Fukwe za Bahari na visiwa vya kuvutia vya Bahari, Aliwahakikishia
waandaaji ushirikiano wa Hali na mali,ulinzi na ukarimu kwa wakati wote
watakapo kuwepo kambini ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)