Picha Zote zinaonyesha Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa
wanatembelea Ukumbi wa Kimataifa wa Makumbusho ya Taifa(NATIONAL MUSIUM
THEATRE).
Washiriki
wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na
wa aina yake Tanzania ambao unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii
kupitia kurugenzi ya mambo ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya
Makumbusho ya Taifa jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo
ya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakiwa
katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja,
walishuhudia Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa kuendesha
Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya nyota tano.
Wengi
wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi na wakuu
wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao umekuwa ni
kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na jopo la msafara huo
lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo hao ya kuomba Fainali hizo
zifanyike ndani ya Ukumbi huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na
Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa kuandaa Fainali hizo
katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM THEATRE, alisema kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa
kuwa lengo na nia ya Mashindano ya Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa
kuna uwezekano pia Fainali hizo zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima
Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya Miss
Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa sasa
unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa kisasa na hadhi ya
kimataifa hapa nchini Tanzania.
ziara
hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe
baada ya kuusikia sifa zake kutoka kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
Aidha Chipungahelo amesema kwamba warembo hao
wanatarajia kupanda katika jukwaani baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea
hifadhi za Taifa ambazo ni pamoja na Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha
na Mlima Kilimanjaro watakaokuwa wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia
hali ya Ukumbi huo Rais wa Miss Utalii
Tanzania, Gideon Chipungahelo amesema kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na
sekta nzima ya Utalii kuona Warembo ambao wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa na ukumbi huo hata kufikia kupeleka maombi ya
kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi wa
kisasa na wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM
THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni kivutio kikubwa kwa
sasa katika anga za Burudani na sanaa.
“Ukumbi
ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni jambo
la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni jambo la
kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana sasa, bila shaka
nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa, lakini hata hivyo ni
changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni
na kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona
wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia
nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao ni
faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia
aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa mashindano haya
kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku ya shindano..
Erasto
G. Chipungahelo Rais
– Miss Tourism tanzania Organisation

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)