Kikosi
cha timu ya Marafiki wa Imani, kikiwa katika picha ya pamoja wakati wa
mchezo huo, uliomalizika kwa timu ya NMB kuibuka na ushindi wa mabao 4-3
dhidi ya timu ya Marafiki wa Imani Kajula, mchezo uliochezwa kwenye
Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Mchezo
huo wa kirafiki ulikuwa ni maalum ulioandaliwa kwa ajili ya kumuaga
Imani Kajula, ambapo katika mchezo huo Kipa wa timu ya Marafiki wa Imani,
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini, Frederick
Mwakalebela, alionekana kuwa nyota wa mchezo huo, kutokana na vitu adimu
alivyokuwa akionyesha uwanjani hapo.
Kiungo
mshambuliaji wa timu ya Marafiki wa Imani, Imani Kajula (katikati)
akimiliki mpira wakati akijaribu kumtoka beki wa NMb, Erick Ruyangi,
wakati wa mchezo huo.
Nahodha
wa timu ya Marafiki wa Imani, Shaffy Dauda (wa tatu kulia) akizungumza
wakati wa muda wa mapumziko, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Makipa
wa timu hizo zilizomenyana kwenye uwanja wa Karume, Frederick
Mwakalebela, akipozi kwa picha na kipa wa NMB, Richard Mwalibwa, baada
ya kumalizika kwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)