LESLIE SEKOTSWE AMTISHIA MAISHA “PRINCE” IMMANUEL NAIDJALA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

LESLIE SEKOTSWE AMTISHIA MAISHA “PRINCE” IMMANUEL NAIDJALA

 php31.tmp  
Bingwa wa Botswana katika uzito wa bantamweight Leslie Sekotswe amekuwa mtu wa hatari kiasi kwamba anamtishia maisha bondia Immanuel Naidjala a.k.a “Prince” wa namibai katika mpambano wao utakaofanyika tarehe 20 siku ya Jumatano jijini Windhoek, namoibia.
 Wawili hao wanakutana katika kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF International Title) katika uzito wa Bantam.

 Leslie ambaye alianza ngumi wakati Immanuel akiwa bado kinda ana rekodi ya kuwapiga wapinzani wake kwa KO katika raundi za mwanzo na ameapa kumpa kipigo kitakatifu Naidjala wakati watakapokutana katika Casino ya Country Resort Club jijini Windhoek, Namibia chini ya promota Nestor Tobias wa kampuni ya Sunshine Boxing Productions iliyoko nchini Namibia.
 
 Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Namibia kufanya mpambano wa hadhi ya IBF la kimataifa na wapenzi wa ngumi wa Namibia wamejawa na furaha kutaka kuliona pambano hili litakalowakutanisha mabondia wawili waliosheheni kwa kila kigenzo cha sifa ya juu.
 
 Huu ni mwendelezo wa IBF Afrika wa kuleta mapambano zaidi ya 100 barani Afrika mwaka huu katika programu yake ya Utalii wa Michezo na tarayi nchi mbalimbali zimejipanga kuandaa mapambano kadhaa wa kadha Tanzania ikowamo!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages