KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA KAMPENI YA " TUPO PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO " LEO JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA KAMPENI YA " TUPO PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO " LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Brewries Limited ,Bw.Ephrahim Mafuru akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni mpya ya bia ya Serengeti Premium Lager inayoitwa "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO,ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali na Kampeni hiyo imeanzia Jijini Dar Es Salaam
Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Bw.Allan Chonjo akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari namna kampeni hiyo  "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO",itakavyofanyika katika mikoa yote ya Tanzania
 Baadhi wa wageni waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya TUPO PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO iliyozinduliwa leo na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited  wakiangalia moja ya Tangazo Jipya la Kampeni hiyo kwenye screen Kubwa uzinduzi huo umefanyika katika hotel ya JB Belmonte
Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Bw Allan Chonjo Kwa pamoja na Meneja Masoko wa SBL Bw Ephraimu Mafuru wakishirikiana kwaajili ya kuweza kuonyesha tangazo la kampeni ya TUPO PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO kampeni iliyozinduliwa leo katika Hotel ya JB Belmonte ya jijini Dar Es Salaam
Meneja wa Mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Iman Lwinga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo mbele ya Wanahabari,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya JB Belmonte,Jijini Dar wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kinywaji chake cha Serengeti Premium Lager.Anaaefuatia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bwa.Ephrahim Mafuru,Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo pamoja na Meneja Masoko Mosses Kebba 

.........
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) leo imezindua kampeni mpya za matangazo kuitangaza bia yake maarufu ya Serengeti inayopendwa na idadi kubwa ya watu. Kampeni hizo maalumu ambazo zitajulikana kama Tupo Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio.
 
Akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hizo jijini Dar es Salaam ndani ya JB Belmont Hotel, Mkurugenzi wa Masoko SBL, Ephraim Mafuru amesema kampeni hizo ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru Watanzania ambao wamekuwa pamoja kiushirikiano katika mafanikio ya kinywaji hicho.
 
Alisema Watanzania wanahitaji kuthaminiwa hivyo wameona kwa kuthamini mchango wao kuna kila sababu za kusherehekea katika mafanikio. "Kampuni ya Bia ya Serengeti inatambua mchango wa kila Mtanzania katika mafanikio yake...ndiyo maana imezindua kampeni hii ya tupo pamoja katika shangwe za mafanikio," alisema Mafuru.
 
Naye Meneja wa Bia ya Serengeti, Allan Chonjo akizungumza katika hafla hiyo alisema kampeni hizo zinazoanzia Mkoa wa Dar es Salaam kwa maonesho mbalimbali na burudani zitakuwa zikiendeshwa baa mbalimbali huku zikiambatana na wateja wa kinywaji hicho kujishindia zawadi anuai.
 
Alisema kampeni hizo zitakazoambatana na matangazo kwenye vyombo vya habari, barabarani pia zitasambazwa katika mikoa anuai ya Tanzania, huku wapenzi wa SBL kujishindia pia zawadi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages