Baadhi ya wakazi wa jiji la dar wakiwa kwa wingi kusaidia zoezi la uokoaji na wengine kushuhudia zoezi la uokoaji likiendelea mara baada ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka leo katika mtaa wa zanaki na hindra ghandi
Wasamalia wema wakishirikiana na vikosi vya usalama katika kutoa mbao na baadhi ya vifusi vilivyodondoka mara baada ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka leo maeneo ya mtaa wa zanaki na Hindra Ghandi
Wakazi wa Jiji la Dar wakishirikiana kuondoa vifusi kwaajili ya kuokoa watu waliofukiwa na vifusi mara baada ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka na kusababisha watu zaidi ya kumi na tano kupoteza maisha baada ya kufukiwa na vifusi
Wananchi wakiendelea na zoezi la uokoaji katika eneo la tukio mapema ya leo
Baadhi ya wakazi wa jiji la dar wakifunga minyororo kwenye moja ya kontena lililofukiwa na vifusi baada ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiwa katika zoezi la uokoaji
Usalama uliimarishwa kila kona ya eneo la tukio huku askari wa jeshi la polisi na jeshi la wananchi wakifanya kazi yao ipasavyo
Askari wakifanya kazi yao kuhakikisha usalama unakuepo
Wananchi wakiendelea na zoezi la kuondoa kifusi kwaajili ya kuokoa watu waliofukiwa na vifusi
Gari likitolewa baada ya kuangukiwa na vifusi mara baada ya jengo la ghorofa 15 kuanguka
Vijana Wa JKT wakiendelea na zoezi la uokoaji katika eneo la tukio
Raisi Jakaya Kikwete Akiangalia Jinsi zoezi la Uokoaji linavyoendelea mara baada ya kuwasili kwenye eneo la tukio katika Mtaa wa Zanaki na Hindra Ghandi
Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wakibadilishana mawazo kuhakikisha zoezi linaenda vizuri
Zoezi la Uokoaji likienda huku greda zikifanya kazi ya kusomba vifusi
Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia zoezi la uokoaji kutoka Vikosi vya Uokoaji na wananchi waliojitolea kuokoa uhai wa wenzetu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)