FAINALI ZA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA ZAFANA HAPO JANA NDANI YA LEADERS CLUB - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

FAINALI ZA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA ZAFANA HAPO JANA NDANI YA LEADERS CLUB

Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanaingia katika viwanja vya leaders club hapo jana katika kushuhudia bar itakayoibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha fainali za Safari lager nyama choma
Hili ndio Jukwaa lililotumika katika Fainali za Safari lager Nyama Choma katika viwanja vya leaders club hapo jana

Mmoja wa Majaji akikagua nyama katika Bar ya Asenga kutoka Buguruni wakati wa fainali za kuchoma nyama zilizofanyika katika viwanja vya leaders hapo jana
 Wachoma nyama kutoka katika Baa ya fyatanga kutoka Boko Jijini Dar wakiwa kazini wakati wa fainali za kuchoma nyama zilizofanyika jana katika viwanja vya leaders ambapo Bar ya Titanic iliibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni Moja
 Wakazi wa Jiji la Dar Wakisubiri nyama choma katika bara ya fyatanga kutoka Boko wakati wa fainali za kuchoma nyama zilizofanyika Jana katika Viwanja Vya Leaders
 Wakazi wa Jiji la Dar na Vitongoji Vyake wakiwa wakijisevia nyama choma wakati wa fainali za kuchoma nyama zilizofanyika katika viwanja vya leaders hapo jana
 Wadau wa Nyama Choma wakiwa wanapiga story baada ya kumaliza kula nyama choma huku wengine wakiendelea kusubiri na wengine wakiendelea kula nyama choma katika fainali za nyama choma zilizofanyika jana katika viwanja vya leaders
 Wadau wa Nyama Choma wakisubiri nyama wakati wa fainali za kuchoma nyama zilizofanyika katika viwanja vya leaders hapo jana
 Pia kulikua na michezo mbalimbali kama mchezo wa pool ambao pia safari lager ni moja ya wadhamini wa michezo ya pool hapa Tanzania
 Luiza Mbutu Nyoni akiwa stejini akitumbuiza na bendi yao ya African stars Twanga Pepeta katika fainali za safari lager nyama choma zilizofanyika katika Viwanja vya leaders hapo  jana
 Wacheza sarakasi wakionyesha uwezo wao katika fainali za safari lager nyama choma zilizofanyika katika viwanja vya leaders hapo jana
Baadhi tu ya umati uliohudhuria kwenye fainali za safari lager nyama choma zilizofanyika jana katika viwanja vya leaders Club huku bar Ya Titanic kuibuka mshindi na kujinyakuliza kitita cha Shilingi Milioni Moja

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages